Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dhana nyingine inayovuka mpaka ambayo ni kinyume na iliyotangulia, inakana upande wa kiroho kabisa (kama tulivyoona kwa Alex Resenberg) na kuhafifisha ukweli wote, ikiwa ni pamoja na kila kipengele cha binadamu, na kuvifanya si kitu bali molekyuli tu zinazojongea. Hii pia ni dhana ya kifalsafa au dhana ambayo inategemewa kwa sehemu kubwa na sayansi ya kisasa.
 
Mtazamo wa Biblia, ambao unasisitiza ukweli na umuhimu wa vipengele vya kimwili, kiroho na kiakili vya utu wetu, ni muhimu sana hasa katika kutafuta afya, uponyaji na furaha. Akili na miili yetu ni sahemu zisizoweza kutenganishwa za uwepo wetu, na program yoyote inayotaka kutuletea maisha bora inahitaji kuzingatia sehemu zote za ubinadamu wetu tata na wa ajabu.
 
Afya inajumuisha kila kipengele cha utu wetu. Kuwa na afya njema ni kuwa sawa kiakili, kuwa sawia kimihemko, kuwa mzima kimwili na kupatana na mwumbaji wetu kiroho. Afya inahusika na mambo zaidi ya kutokuwepo kwa ugonjwa, inahusu akili, mihemko, miili, na hali zetu za kiroho.
 
Mwujiza wa uhai
Uchangamano wa ujumla wa utu wetu ulimfanya mwandishi wa Zaburi aandike: “Nitashukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha” (Zaburi 139:14). Mfalme Daudi (ambaye wala hakuwa mwanafiziolojia) aliwezaje kujua kwamba
 
alikuwa ameumbwa “kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha”? Mtu huyu aliandika takriban miaka 3000 iliyopita, muda mrefu kabla darubini na mashine za eksirei, ukiacha zile za CAT na MRI. Daudi hakuwa najua seli ni nini, ukiacha mlolongo wa sehemu zake tata na za ajabu. Alikuwa najua nini kuhusu maana ya kuzaliana kwa seli au mwunganiko wa protini
 
mbalimbali? Wala asingeweza kujua protini ni nini?
Daudi hakuwahi kusikia juu ya DNA, na akili yake isingeweza kuelewa (wala yetu haiwezi, kwa kweli) jinsi mwili mmoja wa binadamu unavyoweza kuwa na mita trilioni 20 za DNA, na kwamba seti kamili ya vinasaba ina urefu wa zaidi ya herufi bilioni 3.5.
 
Alikuwa anajua nini kuhusu chembechembe nyeupe za damu zinazopambana na wavamizi, au kuhusu hatua nyingi za mtiririko wa vimeng’enya vinavyofanya damu igande?
Pamoja na hayo, Daudi alikuwa anajua kiasi cha kutosha kutambua jinsi ilivyokuwa ni muujiza kwa yeye kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…