Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

b02535ab1a6d47c7dc82ebaba74ca448.jpg
 
Ø Protini: Kila seli mwilini ina protini. Ukarabati wa tishu na ukuaji unazihitaji. Wakati kila chakula kina protini kiasi fulani, mazao ya wanyama kama vile maziwa na mayai ni vyanzo vizuri pia, lakini si vyanzo pekee. Jamii ya kunde zina protini bora kabisa.
 
Ø Shahamu: Hivi ni vyanzo vilivyosheheni nishati. Mara nyingi tunakuwa na mafuta mengi kupita kiasi katika milo yetu kwa sababu ya ladha ambayo mafuta hukipatia chakula. Watu wengi huona ni bora wale chipsi kuliko viazi vya kuchemsha. Hata hivyo, vyakula vya jamii ya karanga vikiliwa kwa kiasi hutoa mafuta bora. Mwili unahitaji mafuta kama hayo ili ufyonze vitamini zinazoyeyuka katika mafuta.
 
Ø Vitamini: Sehemu asilia ambazo ni muhimu katika chakula, na zinahitajika na kiasi kidogo kwa ajili ya ukuaji wa kawaida na utendaji kazi. Vitamini nyingi hupatikana kwa asili katika vyakula mbalimbali. Zingine huyeyuka katika maji na zingine katika mafuta na tusipopata za kutosha ugonjwa utokanao na upungufu hutokea.
 
Ø Antioksidanti na Faitokemikali: Sasa, wanasayansi wanatambua mamia ya vitu hivi, mbavyo hulinda mwili dhidi ya magonjwa na baadhi ya athari za uzee. Huwa tunazipata katika nafaka zisizokobolewa, matunda, mboga na jamii ya karanga.
 
Nanasi ni tunda linalopatikana kwa wingi nchini ingawa wengi hawafahamu umuhimu wake katika kuimarisha kinga za mwili, ili kujiweka mbali na maambukizi ya magonjwa kutokana na kupungua kwa kinga za mwili unashauriwa kula tunda hili kukabiliana na tatizo hilo.
 
Back
Top Bottom