Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sampuli ya damu iliyotolewa kwa ajili ya kupima lehemu inaweza kutumika kwa kipimo cha mafuta mwilini. Inashauriwa, wingi wa mafuta usizidi 100 mg/dl ingawa kiwango chochote chini ya 150 mg/dl kinaelezwa kuwa ni salama.
 
IMG_3365.JPG
 
Shinikizo la damu
Endapo shinikizo lako la damu lipo juu unahitaji matibabu ili kukuepusha na magonjwa ya moyo, maambukizi ya kibofu na kiharusi. Kama shinikizo ni la kawaida, unahitaji kufanya vipimo kila baada ya miaka miwili ili kujua maendeleo yako, wataalamu wanashauri.
 
Kwa viwango vya kitabibu, shinikizo la kawaida huwa chini ya 120/80 mm Hg. Kama shinikizo lako lipo juu, utahitaji vipimo mara kwa mara ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.
Vipimo vya shinikizo la juu huchukuliwa mara mbili kwa tofauti ya saa nne. Hii ni kwa sababu shinikizo lililo juu ya 120/80 mm Hg huhitaji kuthibitishwa na kipimo kingine baada ya kile cha awali kilichoonesha hiyo.
 
Back
Top Bottom