Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake. Wakati wa uumbaji mtu alikuwa mkamilifu machoni pa Muumbaji na Ulimwengu. “nitakushukuru kwa sababu nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha” hivyo ndivyo mfalme Daudi alivyoelezea kicho chake kwa Mungu aliyemwumba mwanadamu (Zaburi 139:14). Dhambi iliingia na kwa kuingia kwa dhambi yakaja na mateso ya aina mbalimbali.
 
Moyo husukuma damu kwenda katika viungo vyote vya mwili. Damu inabeba hewa ya oksijeni na chakula kwa seli za mwili. Hewa ya oksijeni inatumika kama nishati ya kuunguza chakula ambacho nacho huzalisha nishati ili kutegemeza seli za mwili. Kama gari linavyounguza mafuta ili kupata nishati ya kuliendesha, seli pia huunguza chakula kwa kutumia hewa ya oskijeni ili kupata nishati muhimu kwa matumizi yake.
 
Mungu katika hekima yake aliumba figo ili kuchuja takataka (sumu) kutoka na kuziondoa mwilini. Damu inaingia kwenye figo kupitia mishipa ya ateri za mafigo. Damu inachujwa na kuondolewa sumu zote. Maji yaliyochujwa yanayeyusha takataka zilizochujwa na kuzalisha mkojo. Mkojo husafirishwa kupitia ureta mpaka kwenye kibofu ili kuhifadhiwa.
 
Wakati kibofu kinakuwa kimejaa (ujazo ni karibu mililita 500), hisia hufanyizwa ambayo husababisha haja ya kutaka kukojoa. Ndipo mtu anakwenda mahali panapokubalika kijamii, na anapokuwa tayari misuli ya kibofu hukaza, na musulibanifu (kilango) hufunguka na shinikizo linalosababishwa na kukaza kwa kibofu hulazimisha mkojo kutoka kupitia katika urethra (ujia wa kutolea mkojo). Wakati kibofu kinapokuwa tupu musulibanifu hufunga na adha ya kibofu kilichojaa inapungua.
 
Wanaume wengi wanapata mabadiliko ya mkojo kadri wanavyokuwa wazee, mabadiliko yanayoweza kusababishwa na uvimbeuchungu au ukuaji wa tezi ya prosteti (BPH) ni moja tu ya sababu za dalili za matatizo katika mfumo wa mkojo. Hivyo hebu nianze kueleza kwa ufupi tezi ya prosteti ni nini.
 
Chini ya kibofu cha mkojo kuna tezi ya prosteti ambayo inapatikana tu kwa wanaume. Kabla ya baleghe tezi hii huwa ni ndogo sana lakini baada ya hapo inaanza kukua kwa kasi kutokana na mchocheo wa homoni ya kiume iitwayo “testosterone”. Ujia wa urethra unapitia katika tezi ya prosteti. Kadiri ya mtu anavyo ongezeka umri tezi ya prosteti inakuwa kubwa zaidi na zaidi. Inaweza kuongezeka ukubwa bila kuwa na ugonjwa ndani yake au
 
inaweza ikakua ikiwa na ugonjwa ndani yake (mfano saratani). Kadiri inavyokuwa kubwa zaidi inaufanya ujia wa urethra kuwa mwembamba. Kubanwa kwa ujia wa kupitia mkojo husababisha matatizo katika kutoa haja ndogo.
 
Je, Ni Matatizo Gani Ambayo Hawa Wanaume Wenye Tezi Kubwa ya Prosteti Hukabiliwa Nayo?

Sio dalili zote za haja ndogo zinatokana na mabadiliko katika tezi ya prosteti. Aidha kuna wanaume wenye tezi kubwa ya prosteti na bado wanapata dalili chache tu za matatizo ya mkojo kama zipo.
 
Dalili za matatizo ya mfumo wa mkojo zinazojitokeza kwa kawaida ni:
a. Mchirizi dhaifu na unaokatizwa wa mkojo.
b. Tatizo la kuanza kukojoa hata wakati kibofu kimejaa.
c. Hisia kuwa kibofu bado hakijatoa mkojo wote.
d. Hitaji la kukojoa mara kwa mara wakati wa mchana na wakati wa usiku.
 
3b7efe2819c561bdf216e5722abad84d.jpg
 
Back
Top Bottom