Wakati kibofu kinakuwa kimejaa (ujazo ni karibu mililita 500), hisia hufanyizwa ambayo husababisha haja ya kutaka kukojoa. Ndipo mtu anakwenda mahali panapokubalika kijamii, na anapokuwa tayari misuli ya kibofu hukaza, na musulibanifu (kilango) hufunguka na shinikizo linalosababishwa na kukaza kwa kibofu hulazimisha mkojo kutoka kupitia katika urethra (ujia wa kutolea mkojo). Wakati kibofu kinapokuwa tupu musulibanifu hufunga na adha ya kibofu kilichojaa inapungua.