Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-08-24-13-05-27.png
 
Harufu mbaya ya kinywa inaweza kuwa tatizo linalokukera hata kukusababishia wasiwasi unapojumuika na wenzako katika masuala mbalimbali, iwe ofisini au mtaani.

Kitu ambacho wengi hawafahamu ni kwamba dawa nyingi zinazouzwa na kuelezwa kutibu tatizo hilo hazina uwezo
 
wa kuleta suluhu ya kudumu bali ya muda mfupi tu. Dawa hizo hazitibu tatizo bali linagusa tu athari zake.

Usishangae kwa sababu ya uwapo wa dawa kadha wa kadha zilizotengezwa kwa ajili ya kupambana na harufu ya kinywa. Dawa hizi hazijaelekezwa kwenye kiini cha tatizo bali linapoishia.
 
Ili kumaliza harufu ya kinywa ni lazima kujua imesababishwa na nini ambacho kitadhibitiwa kikamilifu ili kupata suluhu ya kudumu. Zipo sababu nyingi zinazochangia harufu hii.

Baadhi ya vyakula, magonjwa au tabia huweza kusababisha harufu mbaya ya kinywa. Pamoja na hayo habari njema ni kwamba unaweza kuondokana na kadhia hiyo kwa kufanya usafi madhubuti wa kinywa chako.
 
Back
Top Bottom