Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Harufu mbaya ya kinywa inaweza kuwa tatizo linalokukera hata kukusababishia wasiwasi unapojumuika na wenzako katika masuala mbalimbali, iwe ofisini au mtaani.

Kitu ambacho wengi hawafahamu ni kwamba dawa nyingi zinazouzwa na kuelezwa kutibu tatizo hilo hazina uwezo
 
1
77b0b2d0b406229ab775e31290f7146f.jpg


android phone
 
wa kuleta suluhu ya kudumu bali ya muda mfupi tu. Dawa hizo hazitibu tatizo bali linagusa tu athari zake.

Usishangae kwa sababu ya uwapo wa dawa kadha wa kadha zilizotengezwa kwa ajili ya kupambana na harufu ya kinywa. Dawa hizi hazijaelekezwa kwenye kiini cha tatizo bali linapoishia.
 
Ili kumaliza harufu ya kinywa ni lazima kujua imesababishwa na nini ambacho kitadhibitiwa kikamilifu ili kupata suluhu ya kudumu. Zipo sababu nyingi zinazochangia harufu hii.

Baadhi ya vyakula, magonjwa au tabia huweza kusababisha harufu mbaya ya kinywa. Pamoja na hayo habari njema ni kwamba unaweza kuondokana na kadhia hiyo kwa kufanya usafi madhubuti wa kinywa chako.
 
Ili kukabiliana na tatizo hili inashauriwa kuwa macho wakati wote. Hili litafanikiwa endapo utazifahamu dalili za kuwa na harufu isiyopendeza kutoka kinywani mwako. Lakini ni muhimu kufahamu kwamba harufu mbaya hutofautiana kutegemea chanzo.

Kuna baadhi ya watu wana mashaka na harufu ya vinywa vyao hata kama wana tatizo wakati wapo wenye harufu mbaya ila hawajitambui.
 
Kwa sababu ni vigumu kutathmini harufu ya kinywa chako mwenyewe, unaweza kumuuliza mtu wako wa karibu ili kujiridhisha kama una harufu mbaya ya kinywa.

Ukithibitisha kuwa nayo, ni vyema ukapitia ufanyaji wako wa usafi wa kinywa. Jaribu kufanya mabadiliko ya mfumo wa maisha kama vile kupiga mswaki mara baada ya kula na kunywa maji mengi.
 
Ukiona tatizo linaendelea licha ya kufanya mabadiliko haya, ni vyema ukamuona daktari wa kinywa na meno kwa msaada zaidi.

Ni daktari huyu pekee anapaswa kukueleza chanzo cha tatizo hilo ambalo mara nyingi huwa linatokana na matatizo yaliyomo kinywani.
 
Uchunguzi wa daktari wa kinywa na meno unaweza ukakupeleka kwa madaktari wengine kwa uchunguzi zaidi kama ataona tatizo lako halitokani na hali ya afya ya kinywa chako.

Sababu

Mara nyingi harufu mbaya ya kinywa huanzia mdomoni ingawa vyanzo vyake ni vingi. Ugonjwa wa fizi ni moja ya sababu ya harufu hii kwani husababisha kuvimba na kutoa damu wakati wa kupiga mswaki, kung’ata kitu ama kutema mate.
 
Ugonjwa wa fizi hutokana na upigaji wa mswaki. Wakati mwingine huwa hauna maumivu kiasi kwamba mtu anaweza kuwa nao na asijue.

Kutopiga mswaki ni sababu nyingine. Kama hupigi mswaki na kufanya flosi, mabaki ya chakula yakikaa kwa muda huoza na kutoa harufu mbaya. Ulimi nao unastahili kufanyiwa usafi kwani unafanana na taulo hivyo kushika mabaki ya chakula na kuweza kukaribisha bacteria baada ya kula.
 
Meno ya Bandia

Meno ya bandia yasiyosafishwa mara kwa mara au ambayo hayakai vizuri huweza kuhifadhi mabaki ya chakula na bacteria ambao kwa pamoja huweza kuchangia kuwapo kwa harufu mbaya ya kinywa.

Meno Yaliyotoboka

Meno yaliyotoboka hayasafishiki unapopiga mswaki. Matundu yaliyopo kwenye meno hayo huweza kuhifadhi chakula ambacho baada ya muda huoza na kutoa harufu mbaya.
 
Back
Top Bottom