Kwa sababu ni vigumu kutathmini harufu ya kinywa chako mwenyewe, unaweza kumuuliza mtu wako wa karibu ili kujiridhisha kama una harufu mbaya ya kinywa.
Ukithibitisha kuwa nayo, ni vyema ukapitia ufanyaji wako wa usafi wa kinywa. Jaribu kufanya mabadiliko ya mfumo wa maisha kama vile kupiga mswaki mara baada ya kula na kunywa maji mengi.