Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Japokuwa tatizo hili husababishwa na meno yote yaliyotoboka, lakini ya nyuma (magego) huchangia zaidi kwani mara nyingi watu wengi huwa hawayasafishi. Hawafikishi mswaki kwenye meno hayo.

Kinywa Kikavu

Kwa kawaida mate husaidia kusafisha kinywa na kuondoa mabaki ya chakula hivyo mtu mwenye kinywa kikavu huweza kuwa na harufu mbaya kutokana na upungufu huo.
 
Kwa kawaida kinywa kikavu hutokea usiku mtu anapolala na akiamka huwa na harufu ya asubuhi ambayo huongezeka iwapo mtu huyo alilala kinywa wazi. Hali hii pia huweza kusababishwa na magonjwa ya tezi la mate matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huathiri ufanyaji kazi wa tezi la mate.

Dawa

Baadhi ya dawa zinachangia harufu mbaya ya kinywa endapo zitasababisha ukavu wa kinywa. Lakini kuna dawa nyingine zinapotumiwa kisha kumeng’enywa mwilini hutoa kemikali ambazo humfanya mtumiaji atoe harufu yake wakati wa kupumua.
 
Sijasikia milonge [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tumbaku

Uvutaji wa sigara au matumizi ya bidhaa zozote na tumbaku mfano ugoro au shisha huambatana na harufu ambayo mara nyingi huwa mbaya. Wavutaji wa sigara wana uwezekano wa kupata ugonjwa wa fizi ambao ni chanzo kingine cha harufu mbaya.
 
Vyakula

Kuna baadhi ya vyakula huleta harufu isiyo nzuri kinywani. Vyakula kama vile vitunguu maji, tangawizi na vinginevyo baada ya muda huleta harufu mbaya ya kinywa.

Magonjwa Mengine

Mara chache harufu mbaya ya kinywa huweza kusababishwa na maambukizi sugu ya tezi (chronictonsilitis) ambayo bakteria wanaosababisha pia huchangia harufu mbaya. Halikadhalika maambukizi sugu kwenye pua na koo huweza kuchangia tatizo hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…