Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-08-26-22-07-51.png

Dua la kuku kamwe halimpati mwewe
 
Betri kutokaa na chaji muda mrefu

Hili limekuwa ni tatizo sana kwa simu janja lakini kutokaa na chaji muda mrefu kunatokana na ukubwa/udogo wa betri yenyewe. Betri aina ya Lithium inazalisha umeme kwa kiasi cha Watt 150 kwa kiogramu (150 Watt-hours/Kg) na kiwango hicho ni baada ya kufanyiwa maboresho miaka ya ’90 – yaani kabla hata ya uwepo wa simu janja .
 
Na kila betri inawastani wa idadi za kuishiwa chaji na kuchajiwa…baada ya kuisha chaji na kuchajiwa mara nyingi zaidi moja kwa moja betri linapoteza uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu kama ilivyokuwa mwanzo.
 
Kama simu yako inatumia betri nene basi itahifadhi umeme muda mrefu na kama simu yako inatumia betri nyembamba basi itakuwa inahifadhi chaji muda mfupi (kama simu janja zetu). – ila siku hizi makampuni mengi kama Apple na Samsung wanajitahidi kufanya vitu ndani ya betri viwe vidogo sana bila kuathiri sana kiwango cha chaji —-hili ndilo pia linasababisha matatizo ya milipuko kwa sasa…
 
Kuishiwa nguvu kwa betri

Betri haiwezi kudumu na nguvu yake kama kawaida; lazima itapungua. Hii inasababishwa na mchanganyiko wa kemikali ambao huwezesha umeme kuzalishwa hivyo na kufanya kuta za Lithium kuwa nyembamba za kusababisha uwezo wa betri kupungua. Kuchaji simu mara kwa mara kupunguza sana ubora wa betri.
 
Kulipuka kwa betri.

Betri zinazolipuka zinakuwa na nguvu zaidi kuliko uwezo wa Lithium hivyo kama betri zitapewa nguvu zaidi kuliko Lithium lazima zitalipuka. Betri ikipata joto mpaka kufikia nyuzi joto 80 inakuwa katika hatihati kubwa ya kulipuka.
 
Pia sababu nyingine kubwa zaidi hasa hasa inayohusiana na milipuko ya simu za Samsung Galaxy Note 7 ni suala zima la kutaka kutengeneza betri nyembamba zaidi kutokana na ushindani wa soko katika uletaji wa simu nyembamba zaidi. Utengenezaji huu wa betri nyembamba sana unasababisha sehemu za betri zisizotakiwa kamwe kugusana – kujikuta zinagusana…na hili linasababisha mlipuko mara moja.
 
Ingawa betri la simu limetengenezwa na uwezo wa kuchajiwa mara kwa mara ila inafika muda ambao lazima libadilishwe tuu. Hasa inategemea utumiaji na utunzaji wa betri husika ila mara nyingi betri linaweza kuwa zima kabisa kati ya miezi 6 hadi miaka miwili ya kutumiwa.


Haya ndiyo ya kuangalia ili kutambua muda wa kubadilisha betri lako.
 
Muda wa betri kukaa na chaji umepungua na ata zaidi ya nusu ya mwanzo

Itakapofika muda ambao kiwango cha kupoteza chaji kimepungua kufikia hadi nusu au chini zaidi ukilinganisha na mwanzoni ulipoinunua kwa mara ya kwanza basi ujue haifai tena.

Muda mwingine utakuta simu inaonesha inakiwango cha asilimia nyingi tuu ya chaji alafu ghafla unashtukia imezima, ukiwasha inasema ‘battery low’, badilisha tuu betri.
 
Je unasikia simu inakuwa yamoto sana hasa hasa joto hilo likitokea eneo la betri? Epuka hatari, badili betri mara moja. Pia mara nyingi ikitokea hivi kwa simu utagundua pia ata betri halikai na chaji sana ukilinganisha na zamani.

> Linachukua muda mrefu zaidi kujaa

Betri linatakiwa kuchukua masaa machache tuu kujaa, mara nyingi kwa simu za kisasa ni kati ya dakika 30 hadi masaa mawili hivi.
 
Ukiona kuna tofauti ya masaa kadhaa ukilinganisha na lilivyokuwa zamani basi ujue tayari ndani mwake mambo hayaposawa na hivyo uanze maandalizi ya kununua jipya kuepusha usumbufu wa kuchaji kwa muda mrefu kitu ambacho ni hatari.
 
Hili jambo maarufu kwa watu wengi. Betri zuri si kwa simu ata bali ata kwenye magari, ni betri ambalo pande zote zimenyooka.

Kuonesha uvimbe katika pande yeyote ni dalili ya kwamba betri limeshachoka…yaani limetumika sana au limewekwa katika mazingira mabovu. Ukiona hivi ufanye haraka kununua jipya kwani betri lililovimba huwa na hatari ya kupata milipuko.
 
Back
Top Bottom