Maamuzi ya supreme court of Kenya ni ushindi mdogo kwa Raila na Nasa ila kesho ombi lao la kuikagua IEBC ninahisi litatupwa na likitupwa tegemea Raila na NASA kuanza kulalama
Moja, hawajawakilisha hati ya kiapo ya Mtaalamu au wataalamu wa njia za mawasiliano za kieletronikia kuonyesha muda watakaoutumia kuikagua mitambo hiyo na manufaa yake zaidi ya ushahidi ambao tayari upo mahakamani
Kwanza alidai wangelitumia muda wa siku nne kuikagua mitambo tajwa la ajabu alikiruka kiapo chake na kudai masaa 20 yanatosha na alipoona upinzani ni mkubwa akadai hata masaa manne yangelitosha
Nionavyo, kesho hayo maombi yatakataliwa kwa sababu hizo na ikizingatiwa muda wa kulisikiliza hilo shauri unaisha ijumaa ijayo chini ya wiki kutoka leo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.