Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mfano kuna mtu ni dereva wa gari wa muda mrefu lakini akiulizwa sifa ya gari anayoiendesha huwa haijui. Au Kompyuta ambayo ipo ofisini kwake au nyumbani aitumiayo kila siku, lakini hajui wasifu wake vizuri.
 
Kama inavyojulikana Facebook ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo inatikisa dunia kwa sasa. Licha ya hivyo pia Facebook


wana vipengele vingi sana na bado wanaendelea kutoa vingine vingi ambavyo vinaifanya Facebook izidi kuwa Juu. Hivi Ulisikia Hii: Facebook Waja Na Hello – App Mpya Kwa Simu Za Android
 
Achana na hiyo je ushawahi sikia kuwa unaweza badilisha akaunti yako ya facebook na kuwa page? yaani watu wataanza kuku ‘Like’ baadala ya kuku ‘Add As A Friend’. Najua unaweza ukawa na maswali mawili hapo juu ya kwanini na ni kwa vipi?.. Ngoja nikujibu Yote
 
Kwa Nini Ubadilishe Akaunti Yako Ya Facebook Kuwa Page

Kama unatumia ukurasa wako wa facebook kufanya biashara za mtu au hata kutangaza biashara ya mtu si sahihi ni unakiuka vigezo na masharti. Biashara zote inabidi zifanyike katika ‘Page’ na sio akaunti za kawaida kama unazotumia. Kwa kifupi huruhusiwi kutumia ukurasa wako wa facebook kuwasilisha kitu kingine chochote kisichokuwa kinahusiana na wewe kwa mfano biashara yako.
 
Kutokana na hayo basii unahitaji Page ili utangaze na kuendesha biashara yako. Sasa si vizuri kuanza na moja kabisa. Si unaweza tuu kubadilisha akaunti yako ikawa ndio page yako. Hii itakurahisishia kwa sababu hata watu waliokuwa marafiki zako watakua ndio watu wako wa kwanza kwanza kulike page hiyo
 
Pia kumbuka Facebook inaruhusu akaunti ya kawaida kumiliki marafiki 5000 tuu lakini ukiwa na page hata kufikisha bilioni inawezekana. Sasa baada ya kujua sababu twende tukajua tutafanikisha vipi jambo hili.
 
Jinsi Ya Kubadilisha Ukurasa Wako Wa Facebook Kuwa Page

Kabla ya kuchukua maamuzi ya kuendelea ni vyema kujua taarifa gani zitahama kutoka katika ukurasa wako na kwenda samabamba katika Page yako. — Hapa utajua nini kitabaki na nini kitapotea —
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…