Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usafi ufanyike kila siku katika nyumba hasa chooni na jikoni,Tunaepukana na maradhi na magonjwa mengi tunapozingatia usafi.Vile vile tujue tunapofanya usafi nakusahau mpangilio mzuri wa vitu(kuweka vitu eneo husika) bado hatujaepukana na maradhi/magonjwa au ajali za nyumbani.Mfano umefanya usafi jikoni lakini makabati umeacha wazi,vyombo havijakaushwa na kupangwa panapohusika,choo kipo wazi na kwa wale wanaoweka ndoo chooni utakuta kopo la chooni halipo juu kurahisisha uchotaji wa maji na kuzingatia usafi
 
IMG_3802.JPG
 
badala yake kopo linazamishwa ndani ya ndoo;hapo utategemea nini maana mtu atadumbukiza mkono mzima ili achukue kopo na kuchota maji( mikono ya watu mfano watano yataacha maji salama?)Na je umejikinga na maradhi au ajali( kwa mipangilio mibovu ya vitu)?au ndo unatafuta mvuto pasipo misingi ya usalama wa afya yako.
 
Ni vizuri katika swala la usafi itengwe walau siku mbili katika wiki kufanya usafi wa kila mahala na wa jumla hata kama kila siku unafanya usafi.Kwa wale wanaoenda makazini walau siku moja kwa wiki na uhakikishe umefanya kweli.Ni muhimu kufuata ratiba za kazi kama inavyotakiwa. Usiruhusu ajira yako iingilie na kuathiri maisha ya nyumbani (hasa kwa wanawake) nakushindwa kuilea familia inavyopaswa ikiwemo suala la usafi.
 
Back
Top Bottom