Usafi ufanyike kila siku katika nyumba hasa chooni na jikoni,Tunaepukana na maradhi na magonjwa mengi tunapozingatia usafi.Vile vile tujue tunapofanya usafi nakusahau mpangilio mzuri wa vitu(kuweka vitu eneo husika) bado hatujaepukana na maradhi/magonjwa au ajali za nyumbani.Mfano umefanya usafi jikoni lakini makabati umeacha wazi,vyombo havijakaushwa na kupangwa panapohusika,choo kipo wazi na kwa wale wanaoweka ndoo chooni utakuta kopo la chooni halipo juu kurahisisha uchotaji wa maji na kuzingatia usafi