Kama unataka kuona matokeo mazuri ni lazima ukubali kutoa jasho uandike makala zako mwenyewe ambazo zitakupa manufaa makubwa.
5. Kutokuwekeza gharama stahiki
Kama nilivyotangulia kusema, blog ni kazi inayohitaji kuwekeza gharama fulani ili uweze kuona matokeo mazuri. Ni lazima uwekeze fedha na muda ili uweze kufanikiwa katika kazi hii. Gharama ya muda na kujitoa ndiyo inayohitajika zaidi kwenye blog. Utahitaji muda wa kutosha kuandaa makala (post) zenye tija kwa wasomaji wako. Muda huu utahusisha kutafiti, kupanga, kuandika na kuhariri machapisho yako ili yawe bora kwa wasomaji.