Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye watumiaji wa app ya iOS

Ingia kwenye app na bofya eneo la Me, kisha nenda kwenye Settings
Kwenye orodha nenda na bofya Privacy and content
Angalia na tafuta ‘Receive Direct Messages from Anyone ‘, chagua kuwasha (On) kupokea ujumbe kutoka kwa mtu yeyote na zima kuzuia.
 
Je chaja ikiwa bado imebakia imechomekwa huwa inatumia umeme?

> NDIYO!

Ata pale ambapo haujachomeka simu au kompyuta yako bado umeme unakuwa unatumika INGAWA ni kiasi kidogo. (Kumbuka hapa tunamaanisha pia ya kwamba switchi ya umeme ikiwa ipo imewashwa).
 
Kwa mfano uchunguzi uliofanywa na mtandao wa HowToGeek uligundua ya kwamba kama nyumba ina chaja sita na zote zikawa zimeachwa kwenye umeme basi kwa mwaka mzima kuna uwezekano kiasi cha umeme cha takribani kilowatt (kWh) 2.628 zitakuwa zimetumika.
 
Wakati pia utafiti uliofanywa na mwandishi mmoja wa mtandao wa ZDNet ulitambua ya kwamba kwa chaja moja ya simu ya iPhone ikiachwa kwenye umeme kwa kipindi cha mwaka mmoja itakuwa imetumia kiasi cha kWh 1.5.

Kwa kifupi haijalishi, kikubwa zaidi ni kutambua ya kwamba chaja zitaendelea kunyonya umeme kiasi flani pale zinapoachwa kwenye umeme.
 
Inasemekana pia kwa chaja feki na za chini ya kiwango basi ndio zitatumia umeme mwingi zaidi.

Inakuwaje chaja iendelee kutumia umeme ata pale ambapo simu au kompyuta haijachomekwa?

Chaja zote zina ka’transfoma kadogo ndani yake. Haka ndio kanakuwa bado kameunganisha mfumo wa umeme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…