Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ninaamini tunafundwa mengi kuhusiana na utunzaji wa nyumba na waume wetu katika ndoa au hata kuwa na boyfriend kutoka katika jamii kwa ujumla. Lakini likija katika jambo la kuzaa na uzazi ni kama vile wazungu wanasema ”taboo”. Ni nadra sana kusikia wanawake wanapeana masomo kuhusu uzazi na ukisikia wanaongelea haya mara nyingi wanapoteshana kwa vile wale wanaowahadithia wenzao pia hawana ujuzi au utaalamu unaotosha. Mara nyingi story zinazoongelewa ni za kutishana tu.
 
Ili mwanamke mjamzito aweze kuzaa kwa njia natural anabidi kwanza apate mafunzo ya kutosha kuhusiana na mwili wake kwa kipindi hiki ili afahamu jinsi ya kujitunza na pia ili afahamu kama kuna tatizo au la.

Pia anabidi apate support ya hali ya juu kutoka kwa jamii inayomzunguka na wale watu karibu kwake ili aweze kuwa na confidence ya kukabiliana na uzazi. Mara nyingi kwasababu wanawake wengi hatujui kitu chochote kuhusiana na kuzaa au labor kwa ujumla tunakuwa kama victims tunasubiri tu siku ifike tuende hospital madaktari na manesi wafanye kila kitu.
 
Ila tukiwa na elimu ya kutosha kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya kurahisisha zoezi zima la kuzaa ikiwa ni pamoja na njia natural za kufungua uzazi, jinsi ya kutambua dalili mbali mbali za labor kuanza, ni vitu gani vitatokea na ni vya kawaida, ni vitu gani ni hatari na jinsi ya kukabiliana na mambo haya.
 
Pia kwa sababu ya uoga na kutokufahamu wanawake wengi wanapanga tu kufanya operesheni kwa vile hawafahamu kuna njia natural za kupambana na mumivu ya labor na madhara ya dawa mbali mbali ambazo zinaweza kutolewa wakati wa kuzaa.

Pia support katika familia ni kitu muhimu sana kama hamna mtu katika familia yako anafahamu chochote kuhusiana na hili. Basi inamwia vigumu mwanamke kukabiliana na mambo mbali mbali yatakayotokea na kufanya maamuzi ya busara.
 
Support kutoka kwa familia na elimu au mafunzo pia itamsaidia mwanamke kuweza kuchagua wauguzi wazuri zaidi ambao watakubaliana na maombi yake na kumsikiliza.

Jamii nayo kuzidisha woga kwa mwanamke:

Kila kukicha huwa tunasikia story jinsi mwanamke mwingine alivyopata experience mbaya wakati wa uzazi. Ukimuuliza mwanamke yoyote yule ambaye hajaza au hata yule ambaye amezaa lakini hakuwa na experience nzuri kuwa kwanini wanaogopa kuzaa watakuambia wanaogopa mambo yafuatayo.
 
Maumivu makali ya uzazi na kuogopa labda kitu kibaya kitatokea.

Wengi wanaogopa vitu kama kukatwa huko chini wakati wa uzazi ili kuongeza njia.

Wanaogopa kuchanika wakati wa kusukuma mtoto.

Wanaogopa uke kutanuka na kutorudi katika hali ya kawaida na kuharibu raha au kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa.
 
Hahahaha
acha nipambane na hali yangu na hali ya mwanangu mana nikipambana na watu nitaishia kufanyiwa operation bila ganzi😉😉
 
Wanaogopa mtoto kupatwa na tatizo au kufariki au hata mama kupatwa na tatizo wakati wa kuzaa.

Wanaogopa kujiachia haja kubwa wakati wa kusukuma mtoto. Wengine wanaogopa kuzaa kwa operesheni.

Kwa kweli kuzaa si kazi lelemama na nasema hivi sio kwa kutisha ila tuichukue kama changamoto ya kwamba tujifunze jinsi ya kukabiliana na siku hiyo muhimu ili mwili uweze kufanya kazi yake kisahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…