Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bob12 na Viv? Safi sana [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
e4536fa48fd6b31533249b9e77cce068.jpg
Awesome photo
 
Hizi dawa mara nyingi zitaanzisha uchungu lakini kama mwili hauko tayari basi kutanuka kwa uzazi kutachukua muda na hapo ndio maumivu yatakapozidi kuwa makali na mtoto mara nyingi anakuwa affected na haya madawa basi hapo ndio daktari atabidi ashauri kufanyiwa operesheni. Lakini ukweli ni kwamba hii yote haiko necessary.
 
Kwenye filamu mara nyingi wanaonyesha mtu kashikwa na uchungu maji yamemwagika, kazaa hapo hapo kabla hajafika hospitali. Lakini katika maisha ya kawaida ni nadra sana kutokea. Hasa hasa kwa mtoto wa kwanza. Wanasema kuwa avg ni masaa 12 hadi 17 lakini kuna wanawake ambao wanakuwa kwenye labor siku 3 hadi 4 yaani masaa 72 hadi 96 kuna wale ambao wanabahatika na inakuwa fupi masaa mawili hadi matano hivyo inategemea.
 
Ila kwasababu watu wengi siku hizi hatuna subira na wauguzi wanashughuli nyingi hawawezi kukaa kukusubiria wewe tu mpaka uzae hivyo mara nyingi ikipita baada ya masaa fulani wataanza kukupa ushauri wa kukupa dawa ya kuongeza spidi ya labor hii dawa ndiyo itaongeza spidi lakini ndio maumivu yatazidi na kuwa makali kupita kiasi kwasababu yale maumivu ni ya dawa na sio maumivu asilia hapo ndio mara nyingi mwanamke atashindwa kuvumilia na kukubali operesheni.
 
Kwa wale ambao labor itachukua muda mrefu inahitajika stamina ya hali ya juu ikiwa pamoja na mwili kuwa fit kwa mazoezi, lishe bora na maji ya kutosha ili kuendelea kuwa na nguvu kwa kipindi chote hichi. Hapa kama huna stamina ndio hapo kuna uwezekano mkubwa wa kukubali madawa na hatimaye operesheni.

Kama mwanamke anafahamu haya na kajitayarisha vya kutosha unaweza kuendelea na labor nyumbani mpaka ikifikia stage fulani ya labor. Tutaongelea kwa undani ni stage gani na dalili gani wiki zijazo.
 
Tatizo lingine ni position mbali mbali za kuzaa na kumsukuma mtoto. Kuna position ambazo ukikaa wakati wa labor zinasaidia kutanuka kwa njia ya uzazi kwa urahisi zaidi. Lakini mara nyingi hospitalini huwa unaruhusiwa kufanya position moja tu ya kulalia mgongo huku miguu imetanuliwa wakati hii ni position ngumu sana kwa mama kusukuma na njia ya uzazi kutanuka. Pia watu wengi hawafahamu hizi position za kuzaa kwa sababu ya kukosa mafunzo.
 
Back
Top Bottom