Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5e062946de040a487fe3cadaaf30f804.jpg
 
Kutofautiana kwa mzunguko wa menstruation cycle au mzunguko wa siku za mwanamke. Wanawake wengine wana mizunguko mrefu na wengine wana mizunguko mifupi.
Ukuaji wa kila mtoto ni tofauti, watoto wengine wanahitaji siku zaidi kuendelea kuwa ndani ya tumbo la mama.
Wamama wengine wanapoulizwa lini ilikuwa siku ya mwisho wa hedhi ili kukadiriwa huwa hawana kumbukumbu sahihi.
 
Ndiyo maana tunabidi tuchukulie haya kama makadirio na siyo siku maalumu ambayo mtoto atazaliwa. Mtoto anaweza kuzaliwa siku chache baada au hata wiki kadhaa baada ya siku ya makadirio. Kwa kawaida mtoto anaweza kuzaliwa siku yoyote katika wiki ya 37 hadi wiki ya 43.
Hata mashine maalum za ultrasound huwa zinafanya tu makadirio na haiwezi kukupa siku kamili ya kuzaliwa kwa mtoto.
 
Madaktari wanawezaa kuweka pressure kwa mama kuwa mtoto lazima azaliwe sasa. Na wanaweza kukupa sababu kuwa placenta inaweza kuacha kufanya kazi na mtoto kuzaliwa na madhara au hata kufariki. Lakini kutokana na research iliyofanyika risk ya hii kutokea ni ndogo sana.
 
Mara nyingi kuna risk zaidi kutokea kama daktari ataingilia kazi ya mwili na kuulazimisha kuzaa kabla haujawa tayari. Kama mama hana elimu yoyote kuhusiana na uzazi au hata kama ana elimu lakini hana confidence, support, msimamo na dhamira, na basi kukubali tu yale anayoambiwa na watu, ni rahisi sana kukubali kupewa madawa ya kuanzisha uchungu.
 
Hizi dawa mara nyingi zitaanzisha uchungu lakini kama mwili hauko tayari basi kutanuka kwa uzazi kutachukua muda na hapo ndio maumivu yatakapozidi kuwa makali na mtoto mara nyingi anakuwa affected na haya madawa basi hapo ndio daktari atabidi ashauri kufanyiwa operesheni. Lakini ukweli ni kwamba hii yote haiko necessary.
 
Sababu nyingine ni pale ambapo labor imeanza lakini inachukua kipindi kirefu. Mara nyingi watu hawafahamu kuwa labour inaweza kuendelea zaidi ya masaa 24 kutokana na mtu na mtu.

Kwenye filamu mara nyingi wanaonyesha mtu kashikwa na uchungu maji yamemwagika, kazaa hapo hapo kabla hajafika hospitali. Lakini katika maisha ya kawaida ni nadra sana kutokea.
 
Hasa hasa kwa mtoto wa kwanza. Wanasema kuwa avg ni masaa 12 hadi 17 lakini kuna wanawake ambao wanakuwa kwenye labor siku 3 hadi 4 yaani masaa 72 hadi 96 kuna wale ambao wanabahatika na inakuwa fupi masaa mawili hadi matano hivyo inategemea.
 
Back
Top Bottom