Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

download.jpg
 
Mimi nilikuwa nataka nijue tatizo lililopo kwasasa kwa wanawake wanapoenda kujifungua, njia za uzazi hazifunguki mpaka inafikia hatua mama anaongezewa uchungu ili njia iweze kuongezeka lakini haisadii hili tatizo linakuwa la nini hasa? kwasababu wazazi wetu hawakuwa na matatizo ya kufunguka njia mama akishapata uchungu tu njia inafunga bila shida lakini kwasasa hivi hili ni tatizo kubwa sana kwa wa mama mpaka inafikia hatua mabinti wanaogopa kujifungua kwa kawaida wakiogopa kupata maumivu yake badala yake wanapendelea visu kwa sana.
 
Kuna sababu mbali mbali zinazosababisha wanawake wa siku hizi kushindwa kufunguka kwa njia ya uzazi na kuwalazimu kupewa madawa kuongeza uchungu au hata kutakiwa kuzaa kwa operesheni/visu/ c-section. Hapa nitajaribu kuchambua kila sababu na ni kwa kivipi hili linachangia.
 
1. Mazoezi
Wanawake wa zamani walikuwa wakifanya shughuli nyingi sana kama kutembea kwa muda mrefu ili kufika sehemu wanazotaka. Walikuwa wanafanya shughuli nyingi za ndani na nje ambazo wanawake wengi wa siku hizi hawafanyi. Shughuli hizi zilikuwa ni mazoezi tosha, zilizokuwa zikisaidia mwili wa mwanamke kufunguka na kulegea katika kipindi hiki.
 
Ila wanawake wa siku hizi mara nyingi tunafanya kazi ofisini, tunaenda kwa magari, unafika ofisini umekaa kwenye kiti, umerudi nyumbani unakaa tena kwenye kochi ukila chakula umekaa kwenye meza ya chakula kwenye kiti, kazi nyingi zimerahisishwa na mashine na hata wasaidizi wa nyumba unaishia kulala tu au kukaa tena kwenye kochi mbele ya tv, computer au simu.
 
Siku hizi shughuli nyingi za binadamu zinatumia akili na ubongo zaidi ya mwili. Ndio imerahisisha maisha yetu ya kila siku ila sasa mwili wetu unashindwa kufanya kazi yake vizuri na unakuwa mzembe.

Ndio maana siku hizi tunashauriwa kutenga muda maalum kufanya mazoezi ili kufidia kuupa mwili mazoezi ya kutosha. Na ni muhimu sana kwa mwanamke mjamzito kufanya mazoezi maalum ili kusaidia kupanua na kuongeza njia ya uzazi. Na sio kufanya mazoezi yoyote yale bali yale muhimu ambayo yatasaidia kuongeza na kupanua njia na misuli maalumu ya uzazi.
 
2. Lishe na diet
Siku hizi lisha bora haizingatiwi na watu wengi kama zamani. Kutokana na kubadilika kwa maisha ya kila siku na kurahisishwa kwa upikaji na utengenezaji wa chakula mara nyingi hatupati lishe bora.

Watu wengi utakuta wanaenda kazini wanashindwa kuchagua chakula bora wanakula tu chakula kile ambacho kipo mitaani kwa haraka warudi ofisini. Uongo mbaya vyakula ni vitamu lakini si vizuri kwa afya zetu.
 
Mara nyingi vyakula hivi sio vizuri kwa vile wauzaji wa chakula wanafanya biashara utakuta vyakula hivi vina mafuta mengi na fructose ili waweze kuvitengeneza kwa muda mfupi na kuvifanya viwe na ladha tamu. Vyakula hivi haviko balanced yaani havitoshelezi mlo kamili wenye virutubisho vyote muhimu kwa binadamu hasa hasa kwa mama mjamzito.
 
*(fructose mbaya ni ile ambayo inatumiwa kama sukari na kuongezwa kwenye vyakula viwandani. Fructose ya aina hii sio ya asilia inakuwa imekuwa processed. Siongelei ile ambayo iko naturally kwenye matunda)
Kama mama mjamzito anashindwa kupata lishe bora basi mwili utashindwa kufanya kazi yake vizuri kumtosheleza mama na mtoto.
 
Mara nyingi kinachotokea utakuta mama na mtoto wanaongezeka uzito lakini huu sio uzito mzuri unaowafaa. Hivyo mtoto anaweza akawa mkubwa sana na inawia vigumu kwa njia ya uzazi kutosha.

Mara nyingine mwili wa mama pia unashindwa kufanya kazi ipasavyo kwa vile vyakula vingi vya siku hizi vina kemikali na hormone mbali mbali ambazo si nzuri kwa binadamu na zinauwezo wa kuaffect zoezi zima la kuzaa ikiwa ni pamoja na ufungukaji wa njia ya uzazi.
 
Mama mjamzito anatakiwa achukue hatua maalum kupangilia chakula ikiwezekana aandike kama ratiba na ajaribu kufuatilia chakula gani anakula kuona kama anapata mlo kamili. Pia ajaribu kuandaa vyakula vyote mwenyewe na kununua vyakula amabyo ni organic na natural ambavyo havijaongezwa madawa na kemikali viwandani.

Pia katika hili nilishaongelea virutubisho vinavyotakiwa kwa mama mzjamzito na mlo kamili uweje, kwa maelezo zaidi kwa hili rudini katika maada za nyuma kuhusiana na hili.
 
3.Jamii kutokuwa na subira na wamama wajawazito pamoja na uingiliaji wa wauguzi katika shughuli nzima ya kujifungua.

Kuna mara kadhaa ambapo hospitali inaweza kutokadiria vizuri tarehe za kuzaliwa mtoto. Mama, familia, marafiki na hata madaktari wakifuatilia hizi tarehe kama maandiko kutoka kwa Mungu inaweza ikawa ni tatizo kwa mama mjamzito pale tarehe au wiki ya kuzaliwa mtoto itakapofika halafu mama bado hajaingia labor au kuanza kusikia uchungu wa kuzaa . Utakuta familia na marafiki wanaanza kumuuliza mama mbona mtoto bado hajaja hii haimsaidii mama bali humtia woga na wasiwasi kuwa labda kuna tatizo.
 
Tunabidi tufikirie kama vile ni tunda, hivi sisi tunafahamu ya kuwa lini tunda ambalo liko kwenye mti litakuwa tayari na kuiva? Ni Mungu pekee ndio anafahamu. Mara nyingi tunasubiri mpaka pale limeiva halafu linadondoka lenyewe. Ukijaribu kulitungua kabla halijaiva unakuta chungu na si tamu tena.
 
Kuna watoto wachache wanaweza kuzaliwa kabla ya miezi tisa kuanzia miezi sita hadi wa tisa. Ila wengi wao kwa kawaida huzaliwa katika miezi minane hadi tisa ya uzazi baada ya hapo unaona kuna uwezekano kabisa watoto wengi kuzaliwa kuanzia mwezi wa tisa hadi wa kumi wa uzazi. Na wengine wachache kwenye mwezi wa kumi hadi wa kumi na moja.
Kwanini makadirio ya siku ya kuzaliwa mtoto huwa mara nyingi si sahihi?
 
Back
Top Bottom