10. Hakiki
Nimeshangazwa na matumizi ya App hii na kilichonivutia zaidi ni kwamba katengeneza Mtanzania Mwenzetu. Ni jambo la kujivunia sana, App hii inakuwezesha kufahamu taarifa za matumiza ya pesa zako katika mfumo wa simu (Mobile Money).
Taarifa zako zote za M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na zingine nyingi zinazohusisha pesa katika simu yako kwa mfano ununuzi wa umeme, vocha kwa kupitia njia ya ‘Mobile Money’ utaziona katika App hii. App imetengenezwa na kampuni inayojulikana kama Nabure.