Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

kuwa na mkalimani wako karibu, kumbuka Gooogle Translate inatafsiri lugha zaidi ya 29. Ukiwa na App hii unaweza ukatafsiri lugha kadhaa tena kwa kutumia kamera ya simu janja yako. Cha kufanya ukiona kuna neno la kigeni limeandikwa sehemu chukua simu, fungua App na kisha lengesha kamera katika eneo hilo na Google translate itatafsiri kuja katika lugha unayoitaka.
 
App muhimu sana za kuwa nazo katika vifaa vyako (simu au hata kompyuta) ni hizi. Google Drive au Drop box kazi zake ni moja tuu, zitakuwezesha wewe kuhifadhi mafaili yako katika mtandao na kuyachukua muda wowote unapoyahitaji ili mradi tuu uwe na huduma ya intaneti.

Hebu fikiria kama simu yako imeibwa na ulikuwa umehifadhi vitu kama vile picha na nyimbo katika huduma hizi? Inamaanisha kuwa mfaili hayo unaweza ukayapata tena.
 
Ukiwa na App hii utaweza kulinganisha fedha za kigeni na za nchi yako au nchi nyingine ili kujua ni shilingi ngapi kwa wakati huo. Hivi ni maran ngapi umeuliza au rafiki yako amekuuliza kuwa dola moja ni shilingi ngapi ya Tanzania? Ukiwa na App kama hii maswali kama hayo huwezi ukauliza. App hii ni ya muhimu hata kwa wale ambao wanasafiri nje ya nchi I
 
Android Device Manager

kama ikitokea umepoteza au kifaa chako cha Android kimeibwa ukiwa na App ya Android Device Manager unaweza ukakipata. kinachofanyika hapa App hii itakusaidia kujua eneo la kifaa chako kilipo.
 
Licha ya kuwa unaweza ukajua mahali kilipo bali pia unaweza ukakiloki kifaa hicho kwa kutumia taarifa za akaunti yako ya Google, pia unaweza ukafuta taarifa za kifaa chicho (mfano unaweza ukafuta taarifa zote katika simu). Hata kama una kifaa zaidi ya kimoja App hii itakuwezesha kujua vyote viko wapi kwa wakati huo.
 
9. Google

Moja kati ya App maradufu kabisa za kuwa nazo katika simu janja yako yako ya Android ni Google. Ingawa wengi wataona ni sawa tuu kuingia katika mtandao wa Google kwa kutumia kivinjari (bila kutumia App hii) lakini bado kuwa nayo katika simu janja yako ni vizuri zaidi.

Google itakurahisishia kufanya kazi mbalimbali ambazo huwa unazifanya katika mtandao wa Google kwa haraka zaidi. Hapa utapata taarifa mbali mbali (habari, michezo n.k) kwa haraka zaidi. Pia kama kawaida utaweza kuiuliza Google maswali mbalimbali (haahaha)!. Ili kuipakua katika simu janja yako ya Android inabidi kuingia hapa
 
10. Hakiki

Nimeshangazwa na matumizi ya App hii na kilichonivutia zaidi ni kwamba katengeneza Mtanzania Mwenzetu. Ni jambo la kujivunia sana, App hii inakuwezesha kufahamu taarifa za matumiza ya pesa zako katika mfumo wa simu (Mobile Money).

Taarifa zako zote za M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na zingine nyingi zinazohusisha pesa katika simu yako kwa mfano ununuzi wa umeme, vocha kwa kupitia njia ya ‘Mobile Money’ utaziona katika App hii. App imetengenezwa na kampuni inayojulikana kama Nabure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…