Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hebu jaribu kutembelea kwenye saluni za kike, utakuta hakuna kinachozungumzwa huko zaidi ya kusengenya, tena kibaya zaidi ni usengenyaji wa kubomoa na kuharibu umaarufu wa watu wengine. Kama wamemtembelea mwenzao au kuhudhuria mazishi ya msiba unaomhusu mwenzao, shuhudia mazungumzo yatakayotawala wakati wanarudi.
 
Njia nzima mjadala utakuwa unahusu maisha ya mwenzao, kwamba hana hiki , hana kile, au mazishi hayakuwa mazuri kama ya fulani, pia hata kulinganisha thamani ya jeneza la maiti na umaarufu wa mhusika. Utawasikia wakisema “kuringa kote kule kumbe si lolote wala si chochote, ndani kwake kubaya, hana hata kitu cha thamani ukilinganisha na mavazi yake na umaarufu wake”.
 
Litazungumzwa hili na lile ilimradi tu kumbomoa mhusika. Hivi karibuni niliamua kufanya kautafiti kadogo pale ilipo biashara yangu kwa kuwauliza baadhi ya wateja wangu na wapita njia wengine. Nilizungumza na baadhi ya wanawake pamoja na wanaume kadhaa kuhusu hili suala la kusengenya. Dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sharifa, alithibitisha kuwa ni kweli sisi wanawake tunaongoza kwa kusengenya, lakini alitetea kuwa kuna tofauti ya kusengenya na kumzungumzia mtu au watu kwa mazuri na mafanikio yao.
 
Sharifa alibainisha kuwa sio vibaya kumzungumzia mtu kutokana na mafanikio yake, kwani hiyo kuwapa fursa ya kujifunza kulingana na mafanikio ya mwenzao, pia hata wanapozungumzia mapungufu ya mtu, hiyo ni kwa ajili ya kujifunza kutokana na mapungufu ya mwenzao.
 
Dada mwingine aitwae Bupe, alisema kuwa hata wanaume nao husengenya, yeye alishawahi kumfuma mvulana ambaye punde tu alitoka kufanya naye mapenzi akiwasimulia wenzake jinsi yeye (Bupe) alivyo awapo kitandani, kuanzia mwili wake hadi namna anavyofanya mapenzi.
 
Ukweli ni kwamba hakuamini tukio lile kwa sababu mvulana aliyemwamwini na kuamini kumkubali kuwa mpenzi wake baada ya kumtongoza kwa muda mrefu, angeweza kusimulia yale yote aliyoyasikia. Kibaya zaidi hata wale waliokuwa wakisikiliza ule utumbo walionekana kwa nje, kuwa ni watu wenye busara.
 
Kijana mmoja aitwae Dikupila ambaye anamiliki saluni ya kunyoa nywele jirani na ofisi yangu, kwa upande wake aliyewatetea wanaume kuwa siyo wasengenyaji, kwani hayo ni mambo ya wanawake. “Sisi wanaume kusengenya! Haiwezekani, hayo ni mambo ya wanawake, sana sana ukikuta mwanaume anajadili udhaifu wa mpenzi wake hadharani basi ujue huyo jamaa anamatatizo makubwa ya kiakili” alisema Dikupila.
 
Watu wengi wa jinsia tofauti niliobahatika kuzungumza nao walikuwa wanakiri kusengenya lakini walikuwa wanajaribu kutengeneza fasili ya neno kusengenya kwa namna ya kukidhi haja zao. Kwao kusengenya walisema ni mtu kutafuta namna ya kujifunza kuwa bora kupitia makosa ya wengine. Je tabia hii inaweza kuachwa? Wengi walikiri kwamba siyo rahisi tabia hiyo kuachwa kwani imekuwa ndiyo sehemu ya maisha, kwamba haiwezekani watu kukaa pamoja na kuacha kuzungumza matukio na yanapozungumzwa matukio, ni lazima yatawahusu watu hivyo kujikuta watu wanasengenya.
 
Na tabia hii imejikita kila mahali kuanzia nyumbani, mitaani, hadi maofisini, mashuleni na vyuoni. Binafsi naamini kwamba tabia inaweza kuachwa kwa watu wakijikita zaidi katika kufanya kazi na kuwa wabunifu, hasa maofisini. Kama ni suala la mazungumzo iwe ni ya kuleta ufanisi na tija katika kazi kwani waajiri hulipa mishahara kutokana na ufanyaji wetu wa kazi na uzalishaji.
 
Back
Top Bottom