Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Shaffih Dauda acha kufuga maradhi,fuga kuku upate mayai na kitoweo. . . Na :Haji S Manara Shafih Daud ni mmoja ktk watu wa soka hapa nchini,ni rafiki yangu tunaoongea muda mrefu hususan masuala ya mchezo huu murua,uliyobeba maisha yangu,pia ni kijana mwenzangu tunaoheshimiana sana,kiasi cha kwamba sijawahi kwa namna yoyote ile kukwazana nae,hata kama tunatofautiana kimtazamo ktk baadhi ya mambo, hususan ya Soka. Wengi mnakumbuka sakata la Ramadhan Singano,jinsi lilivyokaribia kuvunja uhusiano wetu,kwa jinsi alivyolivalia njuga bila kuujua ukweli,lakini mwishoe ni yy juzi tu aliandika kuwa Singano anataka kuvunja mkataba wake ambao hadi sasa naamini c HALALI, mkataba ulioidhinishwa na TFF huku akiwa na mkataba na klabu nnayoisemea na kuishabikia Simba SC, lakini hayo yashapita, udugu na uhusiano wetu bado upo pale pale. Hata jana baba yangu mdogo Kassim Manara, aliyepo nchini kwa likizo ya majira ya kiangazi toka aishipo huko Belgium, alitaka kuongea nae kupitia cm yangu,na waliongea mengi, huku akimsifu ni kijana mstaraabu ambae hajawah kukosa kwenda kumsalimia pale Antwerp kule Belgium ama Belige kama waitavyo wacongo,kila apatapo nafasi ya kwenda huko, hakika huyu na Eddo kumwembe ni washabiki wakubwa wa wazee wangu, Sunday na Kassim Manara, hata Eddo alimtembelea mwanasoka huyo mahiri wa zamani na wa kwanza nchini kutikisa nyavu za Santiago Barnabeu,wakati akicheza soka la kulipwa kule Austria. Lakini leo nimeamua kumwambia ukweli *'swahiba'* wangu huyo, ukweli ambao ninaamini ataufanyia kazi kwa haraka,ili kulinda image yake na ya blog anayoiongoza na iliyo maarufu miongoni mwa blogs za michezo nchini. Asubuhi nilimpigia kumweleza dukuduku langu, juu ya makala zinazoichafua klabu na uongozi wa Simba, znazoandikwa na mtu aitwae *Mbolembole*, mtu huyu ni mgeni ktk Soka, simjui,sina rekodi nae zozote, ama za uandishi wa michezo, au hata uchambuzi kama walivyo Shafih na kina Eddo. Mtu huyu kila kukicha huandika vtu vbaya kuhusu Simba, hutuchokoza na kutaka kuaminisha watu Simba ni klabu ya hovyo na inaongozwa na watu wasiojua lolote kuhusu futboll. Anaitumia blog ya Shafih kuidhalilisha klabu yetu .
19379886_1384115215001431_8141250306458517504_n.jpg
 
Back
Top Bottom