Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuku mzima (makange style) Mahitaji Kuku mzima Kitunguu saumu nusu kijiko Tangawizi nusu kijiko Curry powder nusu kijiko Masala nusu kijiko Limao Nyanya 3 Karoti 1 Kitunguu maji 1 Pilipili hoho nusu Chumvi Mafuta Njia Pasua kuku katikati kisha mpake limao na chumvi na kisha acha nusu saa na kisha mkaange kuku mzima kwy mafuta mpk aive awe rangi ya kahawia Kisha pembeni anza kwa kuweka mafuta kidogo kwy sufuria kisha weka kitunguu maji acha iwe na rangi ya kahawia kisha weka kitunguu saumu tangawizi curry powder na masala na kaanga kisha weka karoti pilipili hoho na endelea kukaanga kisha weka chumvi na ikisha ivaa mweke kuku wako kwy huu mchanganyiko aingii pande zote za kuku na kisha epua Kula na chochote ukipendacho ugali wali chips
 
PILAU YA NYAMA YA KUSAGA MAHITAJI mchele vikombe 2 Nyama ya ngombe ya kusaga 1/4 kilo Njegere kiasi Kitunguu maji 3 Kitunguu saumu kijiko 1 cha chai Tangawizi nusu kijiko Pilau masala kijiko kimoja Curry powder 1/2 kijiko Royco 1/2kijiko Beef masala1/2 kijiko Mafuta ya kupikia na chumvi Kachumbari Kitunguu maji 1 Nyanya 2 Tango nusu Limao 1/2 Pilipili 1 Njia Weka mafuta kiasi jikoni kisha weka vitunguu subiri vianze kubadili rangi kisha weka kitunguu saumu na tangawizi baada ya hapo weka njegere ulizozichemsha pembeni na nyama acha kwa muda kidogo kisha weka viungo wako pilau masala,curry powder,royco,beef masala na chumvi kisha acha viungo viingii vizuri kwy nyama ya kusaga na viive kisha weka mchele wako na ongeza maji ya moto kiasi kulingana na mchele wako funika na acha mpk pilau likaukii kw moto wa wastani Kachumbari Katakata vitunguu osha na chumvi na maji kiasi kuondoa ukali kisha katia nyanya na tango kwa style yote upendayo kisha weka chumvi,pilipili na limao changanya tayari kwa kuweka kwenye pilau letu Kwa wapenzi wa mayonase unaweza ukaongeza
 
DAGAA WA NAZI NA MAZIWA Mahitaji Dagaa wa mwanza robo kilo Kitunguu maji 1 Nyanya 3 Pilipili hoho nusu Karoti 1 Tui la nazi zito 1/2kikombe Maziwa fresh 1/2 kikombe Kitunguu saumu na tangawizi1/4kijiko cha chai Royco 1 kijiko Beef masala 1 kijiko Binzari ya manjano1/4kijiko Mafuta kiasi Chumvi kiasi Njia Chukuwa sufuria weka mafuta subiri yachemke kisha weka kitunguu kaanga kidogo kisha weka vitunguu saumu na tangawizi endelea kukaanga upate rangi ya kahawia kisha weka karoti pilipili hoho na nyanya endelea kukaanga kisha weka dagaa zako na weka maji au tui la pili km umetumia nazi ya kawaida kisha weka dagaa zako Baada ya hapo weka viungo wako royco binzari na beef masala na chumvi na ongeza maji au tui la pili funika acha ive kwa muda ukishaona imeiva weka tui lako na maziwa acha kwa muda kidogo. Epua na tayari kwa kuliwa haswa na ugali Enjoy
 
Nyama ya mbuzi choma (simple) Mahitaji Nyama ya mbuzi kilo moja Kitunguu saumu kijiko kimoja cha chai Tangawizi kijiko kimoja cha chai Limao moja Chumvi Mafuta vijiko viwili Njia Chukua nyama yako weka viungo vyote kitunguu saumu, tangawizi limao,chumvi na mafuta na unahakikisha viungo vyako vinaingia vizuri kwy nyama Kisha weka funika na weka kwy friji kwa masaa 7 au usiku mzima ili viungo vyako viingii vizuri kwy nyama Kisha bake 160°c kwa masaa 2 au unaweza kuchoma kwy jiko la mkaa lenye wavu juu kwa masaa mawili hakikisha moto ni mdogo ili aive vizuri. Tayari kwa kula -
 
Kuku wa kuchoma Mahitaji Kuku mzima Kitunguu saumu 1 tsp Tangawizi 1 tsp Limao Binzari ya manjano 1/2 tsp Garam masala 1/2 tsp Curry powder 1/2 tsp Chumvi Mafuta vijiko 2 Njia Chukuwa kuku muweke mahitaji yote kitunguu saumu, tangawizi,limao,binzari ya manjano,garam masala,curry powder,chumvi na mafuta na mpake hakikisha anaingia vizuri kwy kuku na kisha muweke kwy friji chini kwa muda wa saa 6 au hata usiku mzima Kisha washa oven 200°c na muweke kuku wako kwa muda wa saa 1 kisha mpasue katika ili kumfungua ili achomeeke vizuri kwa ndani kwa muda wa dk 35 na tayari na hakikisha anapata yangi nzuri ya kahawia. Enjoy unaweza kula na chochote ni mtamu sana
 
MOROCCAN CHICKEN EGGPLANT AND TOMATOES STEW MAHITAJI 3 vijiko vya mafuta ya kupikia kuku 1 mzima wa kisasa Kitunguu maji 1 Biringanya 4 Nyanya kubwa 5 Maji vikombe 2 1/2 Binzari nyembamba tsp 1 Binzari ya manjano tsp 1 Kitunguu saumu tsp 1 Tangawizi tsp1 Paprika 1 tsp Limao 1 Chumvi kiasi Pilipili manga kiasi NJIA Chukuwa sufuria ya kupikia weka mafuta kisha weka kuku wako na koroga huku unamgeuza kuku akauke maji na anze kupata rangi ya kahawia kisha weka vitunguu ,biringanya na nyanya ulizokataka na acha km dakika 5 na baada ya hapo weka vitunguu saumu, tangawizi,paprika,binzari ya manjano na nyembamba ,chumvi na pilipili manga na koroga mpk ichanganyike vizuri. Kisha kamulia limao na weka maji funika na acha mpk kuku aive na maji ya pungue . Epua na tayari kwa kuliwa na chochote utakachopenda kama wali,ugali,viazi,mihogo,mkate nk. -
 
UJI WA NGANO NZIMA Mahitaji 1. Ngano nzima size unayo penda 2. Unga Wa ngano kidogo 3. Sukari 4. Hiliki 5. Nazi Ya unga / tuwi Jisi yakutayarisha na kupika Step 1. chemsha ngano zako mpaka ziwive 2. Zi chuje maji kama hapo kwenye picture kisha weka pembeni Step 2 . Bandika sufuria kwenye jiko tia maji na unga wagano kidogo koroga kwa mchapo upike uwe kama uji lakini uwe mwepesi Sanaa 2. Sasa Tia tuwi lako / ama mimi natia nazi Ya unga kwenye bakuli Tia na maji ya moto piga na mchapo liwe tuwi . 3. Mimina ngano zako + sukari + na hiliki zipike wacha ziweve zikole kila kitu lakini usiwe mzito uwe mwepesi kwasababu kila ukikaa unakua mzito wenyewe na kama utakuwa na uzito unaweza kutia maziwa ya maji kidogo tu. ENJOY
 
VISHETI VYA JAMUFUTA? Unga Siagi Kungumanga kijiko kimoja Maziwa Nido Bank pd kijiko kimoja Chumvi kiasi Mayai 2 Jam Ufuta Sukari Mayarisho Usanga siagi nachumvi pamoja ikiwa tayari unaweka maziwa, kungumanga, mayai, bp na maziwa unaendelea kusanga mpk viwe kitu kimoja ukiwatari unaweka unga wako unachanganya pmj unga ucwe mngumu wala mlain uwe saiz thn unasuma km chapati unaweka jam ulionganganya naufuta unakunja mara2 usisahau sukari yako penbeni ilisangwa kuwa laini unakata vipande vyasaizi yakisheti unachoma kwa oven ukitoa tu unatia sukari yko juu km unavotia donac . Tayari kwa kul
 
Mikate ya batbut. Vipimo... Vikombe 3 unga mweupe. Kijiko cha kulia kimoja na kidogo hamira. Kijiko maziwa ya nido. Kijiko Sukari. Kijiko chumvi. Kijiko mafuta. Njia... Changanya vitu vyote pamoja na ongeza maji kikombe na nusu au viwili mpaka unga ushikane vizuri. Kata Madonge kama chapati acha yaumke kidogo ikisha yakande yawe kidogo mazito kuliko chapati. Yapike mpaka yavimbe kidogo. Tayari kwa kula -
 
JINSI YA KUPIKA EGG CHOP Mahitaji •Mayai yaliochemshwa 4 •Nyama ya kusaga robo kilo •Kitunguu swaum •Tangawizi •Limao •Chumvi •Pilipili •Breadcrambs •Carry powder •Binzari nyembamba ya unga •Yai moja bichi •Mafuta Matayarisho Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa -
 
Mikate ya vitungu Unga wangano nusu Vitunguu 2 Hamira kijiko kimoja cha Chao Chumvi unakisia Maziwa ya unga vijiko2 Nazi moja Baking poda kijiko cha chai kimoja samli kijiko cha chai kimoja Namna ya kupika Kata vitunguu vyako vyembamba ukisha mimina unga kwenye bakuli uvitie vitunguu vifikiche na unga mpaka vilainike halafu. tia baking chumvi samli na maziwa changanya vizuri ikisha changanyika tia hamira endelea kuchanganya sasa chukua tui lako la nazi anza kuukanda unga mpaka uwe kama. Wa chapati ikisha ugawe madonge 4kwahicho kipimo sukuma upake samli kama chapati urol ukisha sukuma uweke uumuke uchome ukichoma tia mafuta kwanza katika pan kama vijiko vya chakula 2 halafu choma chini ukiiva ugeuze upande wa pili utafanyahivo mpaka umalize mikate yako yote
 
VISHETI VIPIMO: Unga wa ngano kilo 1 Yai 1 Kastad vijiko viwili vya kulia Siagi/samli robo Maziwa ya maji /juice ya chungwa glass 1 na nusu Sukari nusu Bp kiac JINSI KUTAYARISHA Changanya unga na siagi mpk vchngnyike pmj na yai, Tia kastad powder na bp changnya Tia maziwa au juis ya chungwa changanya mpk uwe kitu kimoja Unauponda kidogo tu ucwe mlaini sn au tepetepe Than unafny km vishet vya kawaida ila unakata vdonge kw mkono tu Than unachkuwa kidonge kimoj kmj unapitisha juu ya chujio la tambi Unafny hivo mpk unamaliza kisha unachoma km kawaida ya vihet vyengine kwny karai Unatia shira tayari kwakula
 
Pilau ya nyama Mchele Nyama Tangawizi Mdalasini Uzile Maggi cube Chumvi Ndimu Vitunguu Mbatata Thom Chukua nyama ioshe vizuri tia tangawizi kitunguu thom ndimu na pilipili manga ichemshe mpaka iwe tayari Roweka mchele Kaanga viazi mbatata mpaka vibadilike rangi kisha vitoe weka pembeni Kaanga vitunguu vikishakuwa vyekundu tia mdalasini na uzile uzile unaukaanga kidogo pembeni upate harufu nzuri halfu tia maji kiasi na maggi cube wacha ichemke tia mchele na mbatata ukisha kauka tia nyama uache mpaka uive tayari kwa kula Nb...nyama ichemshe vizuri icive sana
 
Kashata za nazi Mahitaji Nazi zilizokunwa 5 Sukari vikombe 6 Maziwa ya unga kikombe 1 Unga wa cocoa kijiko 1 na nusu Rangi ya pink kijiko 1 cha chai Harufu ya strawberry kjk 1 cha chai Jinsi ya kupika Tia sukari ktk sufuria zito na maji kikombe 1 na nusu chemsha mpaka sukari iyeyuke tia nazi song bila kuacha mpaka maji yote yakauke na ianze kushikana punguza moto kisha tia maziwa endelea kusonga mpaka uone I naanza kushikana kama donge epua haraka gawa sehemu 3 moja weka cocoa nyingine weka rangi ya pink na harufu ya strawberry nyingine Acha nyeupe haraka pakaa mafuta mezani kisha tandaza mchangayiko wa cocoa ukishatandaza haraka chukua msukuma wa chapati upakae mafuta kisha sukuma hlf juu ya mchanganyiko wa cocoa tandaza mchanganyiko wa pink kisha sukuma na juu ya mchanganyiko wa pink tandaza mchanganyiko uliobaki kisha sukuma pembeni parudishie vizuri na mkono Acha ipoe kias kisha kata vipande saiz uipendayo Acha ipoe kabisa
 
MKATE WA UFUTA MAHIJAJI UNGA NAZI MAZIWA CHUMVI KHAMIRA MAYAI 2 MATAYARISHO CHANGANYA VITU VYOTE PIGA KWA MKONO MPAKA UCHANGANYIKE VIZURI UWE MZITO KULIKO WA KAIMATI UKIUMUKA TANDAZA KTK FRYING PAN NYUNYIZA UFUTA CHOMA KWA OVEN MOTO WA CHINI HALAF WASHA MOTO WA JUU SUBIRI UIVE TOA NA TAYARI KWA KULIWA NB UNAWEZA KUCHOMA KW MKAA,WEKA MOTO KIDOGO CHINI ,NA MOTO WA JUU UZIDI KIDOGO - 1
 
MAKORONYA YA MAINI MAINI NUSU KILO MAKORONYA MFUKO 1 PILI PILI BOGA (melikata jembamba na refu) CARROT(mekata nyembamba na refu) MATANGO (mekata nyembamba na refu) MVUJE MAJANI TUNGULE (nimezisaga pamoja na pilipili boga kidogo na carrot) KITUNGUU MAJI KITUNGUU THOMU TANGAWIZI UZILE WA UNGA TOMATO PASTE CHUMVI MAFUTA YA KUPIKIA NAMNA YA KUPIKA chukua maini yakate membamba kama snake chips..yatie viungo...(vitunguu thomu..tangawizi..na uzile..nimetia pia na mvuje majani mawili matatu..) Weka jikoni yaache yachemke yawive..yabakishe na supu nzito nzito. Weka maji jikoni kwenye sufuria..maji kiasi. Yafunike yapate kuchemka upesi. Yakichemka weka makoronya yako yakiwa laini yaepue yachuje...kama unavyochuja tambi. Weka sufuria kavu jikoni...weka mafuta yako kiasi yakipata moto..weka kitunguu maji..kikiwivia brown.. Weka mvuje na matango Baadae weka carrot na pilipili boga Baadae vikiwiva weka mchanganyiko wa tungule baadae weka tomato paste Vikiwiva weka supu yako na maini Iwache ichemke..onja chumvi iwe kiasi Than ikiwiva weka makaroni yako than koroga. Baada ya muda epua..usiyaache yakakauka..yaache na maji maji kidogo. iwache iburudike.. Tayari kwa kuliwa -
 
ROUND DONUTS MAHITAJI 1. UNGA WAGANO MUGI 2 NA NUSU 2. SIAGI VIJIKO 2 KULA 3. CUSTARD KIJIKO 1 KULA 4. ARKI KIJIKO 1 CHAI 5. HAMIRA VIJIKO 1 KULA 6. CHUMVI ROBO KIJIKO CHAI 7. YAYI 1 8. SUKARI NUSU MUGI 9. MAZIWA YA MAJI MUGI 1 JINSI YAKUTAYARISHA 1. KWENYE SUFURIA TIA SIAGI IYAYUSHE KISHA TOWA KWANYE JIKO TIA MAZIWA , ARKI , SUKARI KIJIKO 2 KULA , YAYI , HAMIRA NA CHUMVI KOROGA KWA MCHAPO KISHA WACHA KWA DAKIKA 2. 2. KWENYE HUO MCHANGAYIKO TIA UNGA WAGANO NA CUSTARD KOROGA KWA MWIKO HALAFU NAMKONO FUNIKA WACHA UMUKE. 3. UKISHA UMUKA UKANDE TENA KISHA UFUNIKE TENA KAMA DAKIKA 10. 4. FUNUWA UKANDE TENA FANYA VIDONGE VIDOGO VYA SAIZI KAMA HAPO KWENYE PICTURE SOKOTA KWA UREFU NA KUNJA MARA MBILI NA KISHA ZI TWIST ZOTE WACHA TENA ZI UMUKE KIDOGO. 5. TAYARISHA MAFUTA NA ZI CHOMA WACHA ZIPOWE KIDOGO HALAFU ZITIE KWENYE SUKARI ZI PEPETE ZIKOLE SUKARI KISHA TAYARI KULIWA KWA KAHAWA AMA UNACHO PENDA
 
Back
Top Bottom