Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tambua michango ya wafanyakazi kwenye ukuaji wa biashara yako.
Pamoja na kutoa kipato kizuri, binadamu hawavutiwi na kipato pekee, bali wanapenda kuona wakithaminiwa kwa kile wanachofanya. Tambua michango ya wafanyakazi wako kwenye ukuaji wa biashara yako, na wapongeze na kuwashukuru kwa juhudi zao. Unaweza kufanya hivi kwa kuweka nao malengo pamoja na yanapofikiwa wakapata zawadi fulani au hata kutambuliwa kwa kazi yao bora. Kwa vyovyote vile hakikisha wanajisikia ufahari kuweka juhudi zaidi.
 
Wasaidie wafanyakazi kujiongoza wenyewe.
Ni kawaida kwa mmiliki wa biashara kutaka kumsimamia mfanyakazi kwa karibu sana. Unaweza kufanya hivi ila hii itakuchukulia muda wako mwingi na hivyo utashindwa kukuza biashara yako. Pia wafanyakazi wako ni watu wazima, na hakuna mtu mzima anayependa kuona anafuatiliwa kwa kila kitu.
 
Badala ya kuwafuatilia wafanyakazi wako kwa kila kitu, kubaliana nao majukumu wanayotakiwa kutekeleza kisha wasaidie waweze kujisimamia mwenyewe na kutekeleza majukumu yao. Kwa njia hii watu watafurahia uhuru huu na watakuwa na uzalishaji mkubwa sana.
 
Wajengee wafanyakazi kujiamini na sio hofu.
Waajiri wengi wamekuwa wanajenga hofu kubwa kwa wafanyakazi wao. Watu wanahofia wakifanya jambo fulani au wakishindwa kufanya jambo fulani watafukuzwa kazi. Hii inawafanya watawaliwe na hofu na hivyo kushinda kufanya mambo makubwa na mazuri.
 
Kamwe usiwatishie wafanyakazi kwamba utawafukuza kama ndio njia ya kuwafanya watekeleze majukumu yao, hivyo unawajengea hofu. Kama kuna wafanyakazi ambao hawatimizi majukumu yao, kaa nao na ujue tatizo ni nini. Wakati mwingine hawana uelewa halisi wa kazi yao. Wajengee kujiamini na kuamini kwamba wanaweza na watakufanyia kazi nzuri sana.
 
Makosa ni sehemu ya kujifunza.
Jambo jingine muhimu sana unalotakiwa kufanya wewe kama mwajiri ni kuchukulia makosa wanayofanya wafanyakazi wako kama sehemu yao ya kujifunza. Usitoe adhabu kubwa kwa wafanyakazi wanaokosea, ila jua hilo ni darasa zuri kwao na wakati mwingine hawatarudia tena.
 
Wasaidie waone kwamba kosa wanalofanya wanatakiwa kujifunza ili wasilirudie tena na hii itawafanya kuwa bora. Ila kama utawatishia kwamba wakifanya kosa ni dhambi kubwa, watakazana kuepuka makosa na hivyo kuzuia ukuaji wa biashara yako.
 
Back
Top Bottom