Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwanini unununue laptop ya kawaida wakati unauwezo wa kununua laptop ya 2 in 1 Lenovo Yoga 900 inatumia processor ya 6th-gen Intel Core i7 CPU pamoja na kioo cha 13.3-inch 3200 x 1800 ikiwa imetengenezwa kwa dizaini ya kisasa kabisa, laptop hii inauwezo wa kubadilika kutoka kwenye laptop na kuwa Tablet ikiwa ni moja kati ya laptop yenye muundo unaokubalika sana duniani.
 
Kama ilivyo Macbook laptop hii yenye uwezo wa kioo chenye 3840 x 2160 UHD Touch screen ni laptop bora kwaajili ya watu wanao tengeneza michoro mbalimbali kwenye kompyuta maarufu kama Graphics Designers, laptop hii yenye Processor ya Intel Core i7 CPU pamoja na kadi ya graphics ya Nvidia GTX 960M GPU ni moja kati ya laptop chache zenye uwezo wa ku-edit hata video ya 4K.
 
Kama wewe ni mpenzi wa Michezo ya Kompyuta laptop hii ni chaguo zuri kwaajili yako ikiwa imeboresho zaidi laptop hii inatumia teknolojia ya Sci-fi ikwa pamoja na keyboard bora yenye rangi inayo endeshwa na Processor ya 6th Generation Core i7 CPU ikiwa pamoja na kioo chenye teknolojia ya 4K ambacho kinatumia graphics kadi ya Nvidia GeForce GTX 980M mobile GPU. Hii ni moja kati ya laptop bora za michezo ya kompyuta au game mpaka sasa.
 
Kama unatafuta laptop nyepesi ya bei nafuu Toshiba Chromebook 2 CB35 ni laptop bora kwaajili yako ikiwa na kioo cha 13.3-inch pamoja na teknolojia ya HD display laptop hii ni bora kwa matumizi yako ya kila siku pia laptop hii ina kaa na chaji kwa zaidi ya masaa 10 pale itakapo chajiwa ika jaa kabisa.
 
Kama unatafuta laptop ndogo lakini yenye ubora Asus ZenBook UX303UA ni laptop bora sana kwaajili yako ikiwa inatumia teknolojia ya 1080p touch screen pamoja na processor ya Intel Core i5 CPU laptop hii ni kati ya laptop bora zenye umbo dogo pia laptop hii ina hard disk ya 256GB ikiwa inatumia teknolojia mpya ya SSD, kwa upande wa chaji Asus ZenBook UX303UA inakaa na chaji zaidi ya masaa 8 ikichajiwa ikajaa.
 
Sifa za Dell XPS 13

CPU: Intel Core i5 – i7
Graphics: Intel HD Graphics 520 – Intel Iris Graphics 540
RAM: 4GB – 8GB
Screen: 13.3-inch FH (1,920 x 1,080) – QHD+ (3,200 x 1,800)
Storage: 128GB – 256GB SSD
 
Dell XPS 13 ni moja kati ya laptop bora sana laptop hii imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana pamoja kuwa na uwezo mkubwa wa kukaa na chaji. Laptop hii ina kioo chembamba sana pamoja na processor mpya yenye nguvu ya Intel’s Skylake, hakika hii ndio laptop bora sana ambayo unaweze kununua sasa hivi.
 
Sifa za Asus ZenBook UX305

CPU: Intel Core M3-6Y30 – M7-6Y75
Graphics: Intel HD Graphics 515
RAM: 8GB
Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3200 x 1800) IPS display
Storage: 256GB – 512GB SSD
 
Asus ZenBook UX305 ni moja kati ya laptop bora ambazo zimefanana sana na Macbook basi kama wewe unatafuta laptop ambayo ina muundo mzuri pamoja na nguvu zaidi laptop hii ni bora sana, pia Asus ZenBook UX305 inakaa na chaji kwa muda wa karibia masaa 72 hivyo kama unatafuta jembe la kazi pamoja na muonekano Asus ZenBook UX305 ni kwaajili yako.
 
Toshiba Chromebook 2 ni laptop bora kama unatafuta laptop yenye kioo angavu pamoja na nguvu ya kufanya karibia kazi yoyote. Toshiba Chromebook 2 inkuja na mfumo bora wa uendeshaji wa Chrome OS hii ikiwa inakupa uwezo wa kuinstall baadhi ya programu za Android kwenye laptop yako, kwa upande wa chaji laptop hii inakaa na chaji kutokana na matumizi yako hivyo kama unajua unataka kuitumi kwa muda mrefu ni vizuri kukumbuk kubeba chaji.
 
Sifa za MacBook Air inch-13

CPU: Intel Core i5
Graphics: Intel HD Graphics 6000
RAM: 8GB
Screen: 13.3-inch, LED-backlit glossy display (1,440 x 900)
Storage: 128GB – 256GB SSD
Kama unatafuta laptop ngumu yenye uwezo mkubwa basi MacBook Air inch-13 ni laptop bora kuwa nayo, laptop hii ni nyepesi lakini wepesi wake sio sawa na uwezo wake kwani laptop hii inauwezo mkubwa wa kufanya karibia kila kazi lakini kama ni graphics designer ninge-kushauri kuangalia laptop nyingine kwenye list hii. Kwa upande wa chaji laptop hii inauwezo wa kukaa na chaji masaa 13 hivyo kumbuka kubeba chaja (charger) pale unapotaka kutumia laptop hii siku nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…