Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

e36368d56f153b91d2c0b192f5530226.jpg
 
Sayansi ya Teknolojia ikiwa inaendelea kushika kasi siku hadi siku, chumba hiki maalum kilichojengwa juu ya safu za milima ya Alpine iliyopo Ufaransa kimepata kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wanaotokea sehemu mbalimbali.
 
Unaambiwa sio rahisi kwa mtu mwenye roho nyepesi kuweza kusimama kwenye kichumba hicho kidogo kutokana na kuwa kileleni mwa mlima Alpine takribani umbali wa mita 3800 kutoka usawa wa bahari ambapo utengenezaji wake ulichukua takribani muda wa miaka miwili na ada ya kutembelea kwenye kivutio hicho ni kiasi cha Euro 55 ambazo ni sawa na Tsh 80,000 bila chenji.
 
Kwa mujibuwa shirika la utafiti wa masuala ya anga la nchini Marekani NASA, nimeyapata mambo 6 kuhusu Sayari ya Venus.

Sayari ya Venus ina unga sumaku mdogo kuliko dunia. Inaelezwa kuwa uchache wa ungasumaku husababisha mionzi ya anga ya jua kuingia kwenye angahewa, na mionzi hiyo huzalisha umeme kutokea kwenye mawingu.
 
Venus ikizunguka yenyewe kwa mzunguko mmoja inahitaji siku 243 za dunia, na ikizunguka jua kwa mzunguko mmoja inahitaji siku 224.7 kwenye dunia. Unaona sentensi hii ni ngumu kuielewa? Hii inamaanisha kuwa kwenye sayari hiyo siku moja ni ndefu zaidi kuliko mwaka mmoja!
 
Back
Top Bottom