Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna Mafuta Special Ya Mba Kama Sulphur 8; Au Virgin (Ya Tube) Hayo Ni Kiboko ya Mba Sugu; atumie hayo Kama dawa Yani Kila Siku mfululizo Kwa Kama Mwezi Ndo ataona changes apake mstari Kwa mstari Kwenye ngozi juu Kwenye Nywele anaweza kupaka Mafuta ya Maji Aidha ya NAZI Au atafute VATIKA. Suala Jingine Ni Kuosha Nywele na Shampoo Nzuri za Mba Kama Head and Shoulders Au atafute shampoo za ANTI DANDRUFF; asugue Sana ngozi ya kichwa na Kusuuza na Maji ya Moto. Hii Sio Shughuli ya kufanyia saloon Maana Ni Kama tiba. KUHUSU steaming- Afanye Steaming za Asili; Kwa Mfano Kwa Hali yake- anaweza akatumia Parachichi Moja; Yai Moja akayaponda akapaka kwenye ngozi then aoshe; akifanya bidii ataona mabadiliko.
 
1. ONDOA VINYONGO, MINUNO, HASIRA NA VISASI:
….. katika safari yetu ya maisha hapa duniani yapo mambo na wapo watu ambao hutukwaza kwa kiasi cha kuacha makovu mioyoni mwetu… tunaapa kutowasamehe…. Tunaapa kuwachukia kila tunapowaona….
Mpendwa msomaji!
Kwa imani yangu ya kikristo tumeagizwa kusamehe duniani ili Baba Mungu apate kutusamehe pia dhambi zetu…. Wakati tunapoelekea kuumaliza mwaka ni vema tuitue mizigo hasi chini na kujaza mioyo yetu amani na utulivu wa nafsi….
 
Samehe hata kama hujaombwa msamaha! Msamehe na jisamehe! Na uanze mwezi mpya wa mwisho wa mwaka ukiwa na roho safi isiyo na chochote hasi dhidi ya mtu mwingine! Kukaa na vinyongo, hasira na visasi moyoni dhidi ya mtu hakukusaidii kitu zaidi ya kukufungia mibaraka kwako na kizazi chako!
 
2. OMBA MSAMAHA WA DHATI:
…. Waombe radhi uliowakosea. Wahenga walisema Kiburi si maungwana. Inakufaidia nini kujaa kiburi kiasi cha kushindwa kuomba radhi kwa mtu uliyemuumiza na unajua fika kuwa umemuumiza? Jishushe na umpe mwenzio amani ya moyo! Hakika hata wewe utajisikia amani kupatana na mtu uliyemkosea hata kama hatokusamehe hapo hapo lakini utakuwa umejitoa lawamani.
 
3. ANZA KUANDAA MIPANGO YAKO
…. Binadamu huwa tunapanga ila Mungu huwa ana mipango yake inayompendeza yeye. Pamoja na hili, haituzii kuanza kujipanga. Usisubiri kesho, usisubiri mwakani. Nafasi ya kurekebisha uliyokosa kuyafanya kwa wakati uliopita anza leo kurekebisha japo hata kwa kukaa chini na kupanga ni namna gani utarekebisha…. Usiogope kujikosoa na kuyaona madhaifu yako kwa uwazi. Itakusaidia kupambana na changamoto zijazo…. Yawezekana ulipanga kuwa na biashara yako…. Usingoje krismasi ipite anza leo hii tar 1 kuweka mawazo yako ya wapi uanzie!
 
4. SAIDIA WENGINE WAFANYE WATABASAMU
…. Wasaidie watu wengine kufikia malengo yao hata kwa kuwapa moyo na mawazo chanya. Usishiriki katika kumdidimiza mwenzio… kuna mema mengi Mungu amekufanyia kwa mwaka huu. Hata kama unayapima mema hayo kwa kulinganisha na ya mtu mwingine… bado kuwa na afya njema, kuwa na kama ulivyo, kuwa na watu wako, kuwa hai ni kati ya mema unayopaswa kuyashukuru kwa Mungu na kuyarejesha kwa njia ya kufariji wengine….
 
5. JIPONGEZE
Wengi tunaishi tukiyatafuta maisha na kusahau kuyaishi maisha yenyewe
Jipongeze hata kwa kitu kidogo ulichofanikiwa kukifanya.... Jipe muda ukafanye massage.... toka nenda mahali mbali ukapumzike wewe na wmenza wako au peke yako.
Jinunulie kitu cha kukufurahisha.... jiambie maneno mazuri ya kujenga nafsi .... usikae ukajiambia maskini mimi... kwanini mimi.... sina bahati hiyo na kadhalika. maneno mabaya huumba haraka!
 
5. KIKUBWA TATHMINI UHUSIANO WAKO NA MUNGU!
.... wengi tunajisahau sana katika hili. Tunadhani siku pekee ya kuongea na Mungu ni siku ya kumuabudu… ni wakati unapokwamba tu ndio umkumbuke Mungu…. Jiulize ni Mara ngapi pasipo sababu yoyote umetabasamu ukamshukuru Mungu wako…. Pengine baada ya chakula cha mchana… pengine baada ya kuitazama meza ya ofisi yako…pengine baada ya kutazama watoto wako…pengine baada ya kulitazama gari lako ama tu kwa kujihisi mwenye bahati kuwa hivyo ulivyo, hapo ulipo!.... jiulize ni mara ngapi katika maisha yako umeongea na watu kuhusu Mungu katika namna ya kuwakumbusha uwepo wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…