Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Au kama una watoto basi mchuzi lazima mwenzangu si unawajua watoto kwa mchuzi....otherwise weka tui lako zito utengeneze roast tu.

- igeuze tu mpaka utaona inachemka...dakika mbili zinatosha
zima jiko ila endelea kugeuza geuza mpaka utaonamchuzi umetulia uko softiii
 
kuna watu tembele wanaiona kama mboga duni saaana
Wanakosa uhondo kwa kweli..
Ukishachambua vizuri

- Osha tembele lako...wengine wanalianika juani... mie huwa naenda nalo moja kwa moja tu bila kuanika
- Tia sufuria motoni
- weka mafuta ya kutosha...linataka mafuta hili mwenzangu la sivyo utalichukia
ukalalamike matembele so mazuri kumbe upishi wako duni!
- tia kitunguu chako
 
geuza geuza kisha tia nyanya zako na ya pakti kidogo
- weka royco kidogo
- nyanya zikiiva weka tembele lako

-Ligeuze hapo mpaka linywee
weka maji kidogo mnooooo na kisha funika
- sio unafunika unatoka unaenda kubadili chaneli za TV....utaunguza!
- unakuwa hapo hapo unalichungulia kama limeiva
- ukiona bado unaongeza tena maji kidogo...kidogo
 
usimimine pwaa litadoda!
utaona tu linanywea zaidi ndio linaiva
mwisho mwisho kamulia kipande cha ndimu au limao
- geuza dakika mbili tatu

tayari!


Weka mezani.... kama hutakipenda hiki chakula
Baaasi mwenzangu nimekushindwa...wazungu wamejilamba vidole iwe wewe sasa hahahahahaaa

natumaini umemeza hata mate
 
JINSI YA KUKAANGA NYAMA YA NG’OMBE.

Ukaangaji nyama unasumbua watu wengi tu. Wapo wasiojua kabisaaaa na wapo wanaojitahidi hapa na pale lakini ndio nyama inatoka ngumuuu kama kipande cha jiwe Lol… wapo pia mafundi wa kukaanga na akikukaangia lazima ulambe sahani… twende kazi sasa!

Mwaka huu usipijua kupika vizuri baaasi tena!

Ukaangaji nyama hauna kanuni moja. Zipo kanuni nyingi tu za kukaanga nyama na ikatoka poa kabisa, laini na tamu. Mi nakuletea njia mojawapo.
 
MAHITAJI... itategemea na kiasi unachotaka kupika
- Nyama

- Kitunguu swaumu

- Kitunguu maji

- Tangawizi... menya na uitwange, au isugue iwe laini

- Limao/ ndimu/ vinegar

- Chumvi

- Binzari ya pilau/ binzari masala/ curry powder/ meat masala na vingine unavyopenda

- Pilipili manga
 
- Pilipili manga


- Mafuta kiasi cha kutosha



JINSI YA KUKAANGA

1. Osha na katakata nyama yako katika vipande vyenye ukubwa unaotaka



2. Weka nyama yako kwenye chombo safi kisha tia Limao/ ndimu au vinegar. Chagua kimojawapo. Weka vitunguu swaumu ulivyotwanga na uchanganye na nyama vizuri.
 
Weka viungo vyako unavyotumia, iwe binzari ya pilau, binzari masala, chichen masala, royco au kiungo chochote unacoaka kutumia kuleta ladha murua...mimi hutumia Binzari masala. nyunyuzi pilipili manga kidogo sana kama hupendi ladha ya pilipili kisha tia chumvi!

Changanya vizuri kuhakikisha nyama imechanganyikana na viungo vyako barabara
 
3. Hatua hii inayofuata si muhimu sana ila wapo wanaoipitia....watu huweka tomato sauce, au nyanya za kopo kwenye mchanganyiko. Kisha weka kwenye friji kwa dakika 40... kuweka nyama kwenye friji kwanza husaidia viungo vyako kuingia vyema kwenye nyama na pia hulainisha nyama. hii ni moja ya njia za kufanya nyama itoke lainiiii.... unaweza kuitumia hata katika ukaangaji kuku.
 
4. Baada ya dakika 40 kupita toa nyama yako kwenye friji na ubandike sufuria lenye mafuta kiasi kukaangia nyama yako. usiweke mengi sana!

5. Mafuta yakishapata moto.... kuwa makini kidogo mafuta yasipate moto saaaana kiasi kwamba ukiweka nyama zinacharuka, dakika mbili zinaungua huku hazijaiva
 
6. Mafuta yakipata moto tia vitunguu vyako, vikaange kidogo kisha tia nyama yako geuza geuza kwa muda kisha funika. mvuke unaotokana na kufunika unaivisha nyama vizuri sana. igeuze geuze mara kwa mara ili kuepusha kushika chini. na kama inashika sana unaweka maji kidoooogo kisha unafunika.

unaweza ongeza mafuta kwa kadiri ya wingi wa nyama yako


7. Kama utapenda wakati inakaribia kuiva katia karoti na pilipili hoho hoho kubwa kubwa ukichanganya hoho nyekundu na kijani inapendeza sana na ugeuze geuze mara kwa mara.
 
utaona kama mafuta yanaishia hivi na nyama inaanza kushika kwenye sifuria. cheki nyama yako kama imeiva kama bado ongeza tena maji kidogo sana. usimimine puuuuuu anhaaa! utaharibu pishi lote halafu uje unisingizie sikukuelekeza vizuri hahahahaaa

nyama itajikaanga mpaka ubaki wewe na sufuria na mwiko...bila maji na mafuta kidogo

Ipua nyama yako uichuje kwenye chujio mafuta yadondoke.


Baada ya yote hayo mlo wako unakuwa tayari.... ulie kwa chipsi...ulie kwa pilau...ulie kwa ugali yote heri!
 
The PSG attacker didn't hold back in his criticism of the Catalan club's head man in a comment on social media.
Neymar has slammed Josep María Bartomeu on Instagram, calling the Barcelona president a "joke" for comments made about the Brazil star's father.
 
The 25-year-old completed a move to Paris Saint-Germain last month after the French side paid his €222 million release clause, shattering the record for the most expensive signing in history.
Bartomeu was clearly left dismayed by the antics of Neymar and his father and agent Neymar Santos Sr., who was a driving force behind the move to Paris.
 
We made the mistake of trusting Neymar and his father too much," Bartomeu said.
When an Instagram account posted Bartomeu's quote, Neymar couldn't help but respond in the comments section, saying: "This president is a joke".
 
30734fd4dd6b7f339f88b5afff206264.jpg
 
Mlo wetu wa leo ni UGALI, DAGAA MCHELE za nazi na TEMBELE. Hapo penye ugali unaweza ukaweka wali au hata ndizi za kupika wewe tu upendacho.

TUANDAE UGALI…
Japo najua wengi tunajua kuusonga ugali ila huwezi jua labda wapo wasiojua kuusonga ugali. Acha tuelekezane tu.

- Bandika sufuria lako la maji ya ugali yachemke

- Koroga unga mimina kwenye maji…usikoroge mwepesi sana wala mzito sana

- Sasa uji uchemke, wengine stage hii wanaisha tu basi para para nguna hilo mezani
- Uji ukichemka vizuri hata ugali utatoka poa
Duuuh

CANTSTOPWONSTOP
 
Back
Top Bottom