Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika eneo la Atlantiki kimbunga huitwa hurikan (Hurricane), Pasifiki huitwa taifuni (typhoon) na Bahari Hindi saikloni (cyclone).

Vimbunga hutokea mara kwa mara katika kipindi cha joto. Wataalamu wa hali ya hewa tumeanza kuvipa majina kwa kurahisisha maelewano. Katika eneo la kila bahari kuna utaratibu wa pekee wa kutolewa majina kwa vimbunga kufuatana na mapatano ya wanasayansi.
 
Atlantiki inaona takriban vimbunga kumi au zaidi kila mwaka. Hupewa majina kufuatana herufi A,B, C, ... Imekuwa kawaida tangu 1979 kutumia majina ya kiume na ya kike kwa kubadilishana. Zamani vilipewa majina ya kike tu, lakini wanawake walilalamika.
 
IMG_3867.PNG
 
Wataalamu wanatumia orodha sita ya majina hivyo jina linaweza kurudia baada ya miaka sita. Mfano Kimbunga ca Katrina kilichoharibu mji wa New Orleans, Agosti 2005 kilikuwa cha 11 cha mwaka 2005. Kilifuata vimbunga Jose, Lee na Maria.

Iwapo kimbunga kinasababisha uharibifu mkubwa jina lake huondolewa katika orodha maana kwamba halitarudia.
 
Katrina imebadilishwa kuwa katika orodha ya mwaka iliyotumika mwaka 2011. Hiki kilichotokea karibuni na maeneo ya ukanda wa mwambao wa Tanzania.

Kimbunga kilichotokea karibuni na kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa ni Machi 28, 2014 kilichotokana na mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la Rasi ya Msumbiji Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi.
 
Upepo wake ulianza kuimarika zaidi na kusababisha kuwepo kwa makutano ya upepo na mwelekeo wa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini.

Machi 29, 2014, mgandamizo huo wa hewa uliimarika zaidi na kuwa kimbunga kilichopewa jina Hellen.
 
Upepo wake ulianza kuimarika zaidi na kusababisha kuwepo kwa makutano ya upepo na mwelekeo wa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini.

Machi 29, 2014, mgandamizo huo wa hewa uliimarika zaidi na kuwa kimbunga kilichopewa jina Hellen.
 
Uchambuzi ulionyesha kuwa kimbunga Hellen kilitarajiwa kuongezeka nguvu na kusababisha angezeko zaidi la mvua na upepo mkali.

Hivyo maeneo kadhaa yalitabiriwa kuwa na athari zaidi za mabadiliko hayo kuanzia Machi 30 hadi Aprili mosi 2014.
 
Maeneo hayo ni mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Unguja, Pemba, Dodoma, Singida, Ruvuma, Katavi, Njombe, Iringa, Mbeya na Morogoro.

Viwango vya mvua zaidi ya milimita 50 kwa saa 24 zilizopimwa Machi 30 hadi asubuhi Aprili mosi. Viwango vya milimita za mvua zilizonyesha ni Morogoro 71.9, Mahenge 70.2 na Ilonga 64.7.
 
Katika kipindi hicho nguvu ya kimbunga Hellen ilibadilika mara kwa mara na katika vipindi vifupi hususan kilipokaribia pwani ya kaskazini magharibi mwa kisiwa cha Madagascar.

Hali hiyo ilibadili pia mifumo ya hali ya hewa na viwango vya mvua vilivyotarajiwa katika baadhi ya maeneo ya Tanzania.
 
Kimbunga kinaweza kusababisha hasara kubwa zikiwepo meli, boti na majahazi baharini. Hatari nyingine hutokea kimbunga kinapoyafikia maeneo ya nchi kavu hasa ya mwambao.

Hatari zake hutokana na kasi ya upepo pamoja na kiasi kikubwa cha mvua. Kasi ya upepo inaweza kung’oa vitu vizito kama miti, paa za nyumba au magari na kuvirusha mbali.
 
Hatari nyingine ni ile ya kusababisha vifo. Wingi wa mvua husababisha mafuriko na mvua huwa kubwa sana kwa kiasi cha kusababisha hali mbaya ikiwa ni pamoja na kuharibu miundo mbinu ya barabara na mifumo ya usambazaji wa umeme.

Hali hiyo huweza kusababisha pia uharibifu wa mazao shambani, mifugo na pia milipuko ya magonjwa kama malaria, kipindupindu na kuhara.
 
Kwa wastani kimbunga husababisha maafa na hivyo kugusa na kuathiri kwa kiasi fulani maisha ya watu katika eneo husika. Mvua inayoandamana na kimbunga huvuruga mfumo mzima wa msimu wa mvua katika ukanda wa nchi.

Kabla ya kutokea kimbunga Idara ya Hali ya Hewa hutoa taarifa na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari na mamlaka mbalimbali ili kuwahadharisha.
 
Tahadhari ya mambo yahusuyo hali ya hewa na majanga ni mambo ambayo mtu yeyote anapaswa kuwa mwangalifu na hata kufuata maelekezo ili kuepuka madhara. Kwa kuelimika na elimu inayotolewa na wataalamu wa hali ya hewa, mtu aweza kunusuru maisha.
 
Back
Top Bottom