Watu wengi huingia katika mkumbo wa kunywa pombe kwa namna ambayo ni hatari kwa afya zao. Kuna madhara ya papo hapo na yale ya muda mrefu. Mfano wa madhara ya papo hapo ni ajali, ,kutapika, kuhisi hali mbaya mwilini, kupoteza fahamu na hata kufa. Madhara ya muda mrefu yaweza kuwa kudhoofika mwili kwa kupoteza virutubisho, na kupoteza hamu ya kula, magonjwa ya ini kama kansa ya ini (hepatoma), magonjwa ya figo na ya moyo, kisukari, magonjwa ya akili nk. Hata hivyo kuna mbinu kadhaa za kuepuka madhara hayo kwa kiasi cha kuridhisha. Mbinu hizo ni kama ifuatavyo,