Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unywaji wa pombe ni suala la kihistoria,pombe imekuwa ikitumiwa katika jamii nyingi kote duniani toka karne na karne kama kinywaji na kiburudisho. Ukiachia kuburudisha pombe imekuwa na madhara mengi kwa binadamu kuliko faida zake ukiachia umaarufu na matumizi yake kuwa mkubwa sana.
 
Pombe ina athari hasi kiafya,kiuchumi na kijamii. Pombe inajenga kasumba ambayo inamfanya mtumiaji kujisikia kuihitaji na kuitumia mara kwa mara na hivyo kujenga utumwa wa aina fulani kwa kinywaji hiki.

Bila shaka kwa kujua madhara yake pombe imetajwa kuwa kitu kibaya na kukatazwa katika mafundisho ya dini zote kubwa duniani ambazo misingi yake imejengwa katika kusimamia maadili mema.
 
Wataalamu wanasema uwezo wa wanawake na wanaume katika kunywa na kuhimili pombe unatofautiana. Wanaume wanatajwa kuhimili pombe zaidi kuliko wanaume. Unywaji wa kawaida wa pombe ambao una madhara kidogo unasemwa kuwa ni glasi au bia moja (14 gm za kilevi) kwa mwanamke na glasi au bia 2 (28 gm za kilevi) kwa mwanaume, unywaji zaidi ya hapo unatajwa kuwa unywaji wa kupita kiasi na ndio hasa unaoleta madhara zaidi kama ambavyo yunaeleza katika makala hii.
 
Hata hivyo wataalamu wa afya wanaeleza baadhi ya watu kutotumia pombe kabisa:

Wajawazito au wale wanataka kupata mtoto
Wagonjwa wanaotumia dawa
Waathirika wa baadhi ya magonjwa ambayo pombe italeta madhara zaidi kama ukimwi,kisukari n.k
Watu ambao wanafanya au wanapanga kufanya kazi zinazohitaji kufikiria au kuwa na fikra timamu kama kuendesha gari na mitambo,kusoma au kupanga mambo.
 
1. Madhara ya Unywaji wa Pombe Kiafya
Ni jambo lisilopingika kuwa pombe ina athari mbaya kwa mtumiaji na ni kitu ambacho usipokitumia kabisa au ukiacha kukitumia utapa faida za kiafya



Madhara ya Muda Mfupi

Unywaji wa pombe wa kupita kiasi una madhara ya moja kwa moja kwa afya ya binadamu anayetumia. Baadhi ya madhara hayo ni kama ifuatavyo:
 
Kuharisha
Kutapika
Maumivu ya kichwa
Kuumia kutokana na ajali za magari au pikipiki,kuanguka na kuungua
Ukatili,kujinyonga,ubakaji na ugomvi
Kuathirika na sumu katika pombe kutokana na kilevi kilichopitiliza
Tabia hatarishi kiafya kama kufanya mapenzi bila kinga au kuwa na wapenzi wengi wa nje.
kutoka kwa mimba kwa wanawake au kuza watoto kabla ya wakati
Hupunguza hamu na uwezo kujammiana
 
Madhara ya Muda Mrefu

Matumizi ya muda mrefu ya pombe yanapelekea kupata magonjwa sugu na madhara mengine kiafya yakiwemo:

Msongo mkubwa wa damu-Presha na magonjwa ya moyo
Magonjwa ya ini na magonjwa ya mfumo wa chakula
Kansa ya matiti,mdomo,koo,ini na kansa ya utumbo
Kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kujifunza (Sababu ya ukosefu wa Vitamini B1)
Matatizo ya kiakili-Kukosa dira katika maisha ya mbele (Depression)
 
Kujenga kasumba ya kutumia pombe (Utumwa wa matumizi ya pombe)
Vidonda vya tumbo
Kuongezeka kwa uzito-Kutokana na kiwango cha wanga katika pombe
Ugonjwa wa mifupa(Osteoporosis)-Pombe inapunguza uwezo wa kalsium kutumika kujenga mifupa
Matatizo ya Uzazi-Wanaume wanapungukiwa nguvu za kiume na wanawake kushindwa kushika mimba kirahisi.
Kunywa pombe kidogo kunaweza kupunguza kwa mkiasi kikubwa madhara haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…