Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unaweza kuchukua beseni na kuweka maji ya uvuguvugu yenye povu la sabuni maalum ya kuoshea miguu kisha loweka miguu na iache kwenye maji kwa muda wa robo saa hivi.

Chukua aina ya scrub uliyoichagua kwa ajili ya miguu yako paa na ikikauka anza kusugua miguu yako na hadi kwenye vidole na unyayo.
 
Kisha jisafishe kwa maji ya uvuguvugu.

Baadhi ya vitu unavyoweza kutumia ili ku kutengeneza miguu yako ni pamoja na foot file, Therapysa virgin vie salt scrub, Pedicure iliyotengenezwa kwa OPI Refresh Cooling ffot Gel, Innoxa cool na Calm liquid talc na Feet first reviving Foot Soak.

Bidhaa hizi unaweza kuzipata kwenye duka kubwa la vipodozi na pia utpata maelezo jisi ya kutumia
 
Kisha jisafishe kwa maji ya uvuguvugu.

Baadhi ya vitu unavyoweza kutumia ili ku kutengeneza miguu yako ni pamoja na foot file, Therapysa virgin vie salt scrub, Pedicure iliyotengenezwa kwa OPI Refresh Cooling ffot Gel, Innoxa cool na Calm liquid talc na Feet first reviving Foot Soak.

Bidhaa hizi unaweza kuzipata kwenye duka kubwa la vipodozi na pia utpata maelezo jisi ya kutumia
 
Pia unaweza kutembelea baadhi ya saluni ambazo zinatoa huduma hiyo jitahidi hata mara moja kwa mwezi kuhakikisha miguu yako inapata huduma nzuri ili iwe ya kuvutia.

Kwa wale ambao miguu yao ni makovu au madoadoa wajaribu kutumia scrub na kama hawatafanikiwa kuondoa tatizo hilo basi wanashauriwa ktumia cream na sabuni zenye mchanganyiko wa ukwaju kwani zinasaidia sana kuondoa madoa.
 
Pia unaweza kuchukua mkwaju ukaloweka kwenye maji ukishalainika changanya mchanganyiko huko na asali kasha paka.

Husaidia kuondoa madao na hata kwa wale wenye ngozi za mafuta na chunusi sugu mafuta yatakauka na chunusi hazitatoka tena.
 
Miguu kama sehemu nyingine za mwili isipoangaliwa vizuri huweza leta madhara kiafya. Ni vizuri miguu ikatunzwa vizuri kuanzia viatu vinavyovaliwa hadi jinsi ya kuisafisha. Kuna aina mbalimbali za viatu mfano viatu vya kufunika vifupi, viatu virefu vya wazi, viatu vifupi vya wazi na viati virefu vya kufunika. Viatu vyote hivi huwa vinakuwa na muundo tofauti kadiri mvaaji anavyopendelea.
 
Miguu kama sehemu nyingine za mwili isipoangaliwa vizuri huweza leta madhara kiafya. Ni vizuri miguu ikatunzwa vizuri kuanzia viatu vinavyovaliwa hadi jinsi ya kuisafisha. Kuna aina mbalimbali za viatu mfano viatu vya kufunika vifupi, viatu virefu vya wazi, viatu vifupi vya wazi na viati virefu vya kufunika. Viatu vyote hivi huwa vinakuwa na muundo tofauti kadiri mvaaji anavyopendelea.
 
Ni vizuri kuepuka kuvaa viatu virefu sana mara kwa mara na hasa kama unatembea navyo kwa muda mrefu maana husababisha matatizo kwenye misuli ya miguu kama vikivaliwa mara kwa mara na kwa muda mrefu. Pia ni vyema kutovaa viatu vya kufunika na vyenye joto sana kwa muda mrefu hasa sehemu zenye joto kali maana huweza leta matatizo kwenye miguu. Vile vile si vyema kuvaa viatu vya wazi nje kama sehemu inabaridi kali na barafu.
 
Ili miguu yako iweze kuwa na uzuri wa asili siku zote basi ni vizuri angalau mara moja kwa wiki uwe na siku maalumu ya kusafisha miguu yako (sio kwamba siku nyingine husafishi, la hasha hapa naongelea usafi maalum). Andaa maji ya uvuguvugu na uweke nyenye beseni pamoja na sabuni ya maji ambayo ina dawa (medicated). Kisha kata kucha zako vizuri na kama utapendelea basi uisugue miguu yako kwa kutumia mafuta maalumu ya kusugulia kuanzia kwenye magoti hadi vidoleni (scrub).Kisha loweka kwenye maji kwa muda wa dakika tano.
 
Baada ya hapo nawa vizuri na kusugua unyayo kwa kifaa maalumu au jiwe laini kisha suuza miguu yako na maji safi. Baada ya hapo kausha vizuri na upake mafuta mazuri kwa ajili ya kulinda ngozi ya miguu. Hakikisha uchafu wote umetoka na hasa kwenye kucha na vidole.

Tunza miguu yako vizuri maana ni zawadi kutoka kwa Mungu.
 
Tumekuwa tunatumia muda mwingi kuhakikisha nywele zetu zipo katika hali nzuri na kichwa kwa ujumla lakini tumesahau kuangalia mikono na miguu ambayo ndio mara nyingi huwa ‘bize’ na kazi kwa muda mrefu. Sio lazima uende saluni ili kuhakikisha mikono na miguu yako iko safi na yakupendeza unaweza ukafanya mwenyewe tu nyumbani. Tuangalie jinsi ya kufanya kwa njia rahisi na nyepesi
 
1. Mikono

Ngozi ya viganja vya mikono ni laini na inaweza kudhurika upesi hasa kama unafanya kazi za kutumia nguvu. Ni vuzuri kuhakikisha unaitunza vizuri ili isipoteze uzuri wake wa asili. Inabidi uwe na tabia ya kuifanyia usafi maalumu mikono yako angalau mara moja kwa wiki. Mahitaji ni kama ifuatavyo
 
Losheni ya mikono na kucha
Taulo ndogo
Brash ya mikono
Kikata Kucha
Tupa ya kucha (nail file)
Maji ya uvugu vugu
Sabuni ya maji ikiwezekana medicated
Osha mikono yako vizuri kisha kata kucha kwa urefu unaoona unakufaa na kuzisugua na tupa, baada ya hapo weka maji ya uvugu vugu kwenye beseni dogo na weka matone kadhaa ya sabuni ya maji kisha loweka mikono kwa muda wa dakika tano.
 
Baada ya hapo sugua mikono taratibu hasa sehemu za kiunganishi cha kucha na kidole maana huwa laini sana. Suuza mikono vizuri na maji ya uvuguvugu, kausha na taulo safi na upake lotion ya mikono.

Hakikisha unaitunza mikono yako ili nayo iweze kukutumikia kwa muda wote wa maisha yako haijalishi kama unaitumia kulima, kusuka watu, kuandika au hata kufundishia
 
Kama unatumia mkaa hakikisha unanawa na kusugua mikono vizuri mara tu baada ya kumaliza kuutumia. Kwa ushauri tu unaweza kutembea na lotion yako ili kila unaponawa mikono basi uwe unapaka ili kuhakikisha mikono yako haiwi mikavu. Kama una mtoto mchanga ni vizuri kucha zikawa fupi kabisa kw aajili ya afya na usalama wa mtoto.
 
Back
Top Bottom