Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JINSI YA KUJIOKOA IKITOKEA DHARURA YA MOTO NDANI:

inapotokea dharura ya moto ndani ya nyumba:

1 - Kitu cha muhimu ni kutoka nje salama haraka iwezekanavyo (as soon as possible).

2 - Hakikisha (ensure) kila siku mlango wa dharura (emergency exit) ya nyumba ni umekaa kwa urahisi iwezekanvyo (as simple as possible). Kila mtu ajue funguo za milango ya kutokea zinapowekwa, sio zinafichwa balaa. Have an ermegence exit whenever possible.
 
3 - Fahamu kwamba ktk matukio mengi ya moto (in most cases) kinachoua ni moshi kabla ya moto, hivyo ukiona dalili ya moshi hakikisha unakuwa na kitambaa kibichi cha kujifunika puani na mdomoni, na kama moshi umeanza kuingia ulipo tambaa chini (crawl down) sababu hewa ya uhai (oxygen) ina uzito (density) kubwa kuliko hewa ya kifo (carbon monoxide) hivyo inakuwa imekandamizwa chini sentimita chache kutoka kwenye sakafu (few centimeters from the floor). Hivyo tembea kwa kutambaa.
 
4 - Hakikisha unawajulisha watu wote (Ensure you alert everybody) kama wamelala ili waweze kutoka nje haraka.

5 - Achana na fikra ya kuokoa vitu, ktk hatua hii cha muhimu ni kuokoa uhai kwanza.

6 - Kumbuka, muda ni kitu cha msingi, fanya haraka iwezekanavyo (quick as possible) katika kujiokoa na kuokoa wengine.
 
7 - Ni muhimu nyumba zetu kuziwekea kiashiria moshi (smoke detectors) na pia kizima moto (fire extinguishers). Kugundua haraka (early detection) ya moto ni muhimu sana ili kuweza kuudhibiti kirahisi. Smoke detector ni mashine ya elektroniki ambayo inagundua moshi ktk hatua ya mwanzo kabisa na itapiga kelele (alarm) kwa sauti ya juu, itakusaidia kuamka hata kama upo usingizini na kuweza kujiokoa na kuokoa wengine na kuuzima moto kabla hujashika kasi.
 
KWA NINI WATU WENGINE WANABAKI MASKINI?
Sababu zifuatazo zinaweza kuwa na ukweli
mtupu;
1. Kushindwa kuamua haraka fursa
zinapojitokeza kwao
2. Fursa kali Zikitokea wanaziona kama ni uongo
na utapeli wa mjini
3. Kung'ang'ania kuajiriwa hata kama ajira hiyo
hailipi
 
4. Kudhania unajua sana hivyo huoni jipya la
kujifunza
5. Kukosa ujasiri wa kuanza. Unapanga mwezi
huu au mwaka huu ntafanya hili au lile. Lakini
mwaka unaisha hujaanza!!!
6. Kutokuwa na ndoto ya kiasi cha pesa
unazotaka kwa siku, kwa wiki mwezi au mwaka.
 
12. Kutokuweka akiba yoyote kwa malengo ya
maendeleo ya watoto na wajukuu zao.
13. Kufikiria kuwa kuna siku utapata msaada
kutoka kwa wafadhili, serikali au wazungu au
washikaji zako. Utangoja sana.
14. Kubadilisha mshahara wako au kipato chako
kuwa mali ya ukoo mzima. Kila mtu kwenye ukoo
wenu anakuomba pesa na wewe unampatia.
 
Mshambuliaji Harry kane alifunga mabao mawili huku Tottenham ikiishinda Borussia Dortmund na hivyobasi kupiga jeki matumaini yao ya kombe la vilabu bingwa Ulaya katika uwanja wa Wembley.
Umahiri wa kane mbele ya goli ndio tofauti kubwa waliokuwa nayo Suprs ambao kwa kipindi kirefu cha mchezo huo walilazimika kulinda lango la kutokana na mchezo mzuri ulioonyeshwa na vijana wa Dortmund.
 
Bao lake la kwanza liliwawacha Dortmund bila jibu baada ya kutamba na mpira kutoka upande wa kushoto wa uwanja kabla ya kucheka na wavu dakika 15 katika kipindi cha kwanza baada ya bao la dakika ya 11 la Son Hueng-min kusawazishwa na mshambuliaji wa Dortmund Andriy Yarmolenko.
 
Bao la pili la Kane ulikuwa mkwaju wa kimo cha nyoka katika dakika ya sitini na hivyobasi kuipatia timu yake motisha ya kukabiliana na tishio la wapinzani wao waliotawala mechi hiyo.
Hatahivyo Tottenham walimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji 10 baada ya beki Jan Vertonghen kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumshika mchezaji wa ziada wa Dortmund Mario Gotze.
 
Klabu ya Celtic imeshtakiwa na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya shabiki mmoja kuingia uwanjani na kujaribu kumpiga teke mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe.
Kisa hicho kilitokea katika kipindi cha kwanza cha mtanange huo siku ya Jumanne muda mfupi baada ya wageni hao kuwafunga Celtic bao la tano.
PSG pia inakabiliwa na shtaka la mashabiki wake kuvunja viti vya uwanja huo.
 
Kesi hiyo itaangaziwa na kitengo cha maadili na nidhamu katika shirikisho la Uefa tarehe19 Octoba.
Mkufunzi wa Celtic Brendan Rodgers alisema kuwa amefurahishwa na hatua ya mashabiki kumzomea jamaa huyo aliyeingia uwanjani.
Nadhani hatua iliochukuliwa na mashabiki kumzoma jamaa huyo ilikuwa jibu zuri.
Inakatisha tamaa katika uwanja wowote wa klabu yoyote unapoona shabiki anaingia katika uwanja kama alivyofanya
 
Klabu ya Celtic ilipokea kichapo kikubwa zaidi nyumbani huku Neymar akiiongoza PSG katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Neymar ambaye ndio mchezaji ghali duniani aliifungia timu yake mpya na kusaidia kupatikana kwa bao la pili ambalo lilifungwa na Kylian Mbappe.
Edison Cavani alifunga bao la tatu kwa njia ya penalti na hivyobasi kuwahkikishia wageni hao uongozi kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza.
 
Bao alilojifunga Mikael Lustigs lilifuatiwa na bao la pili la Cavani ambalo lilifungwa kupitia kichwa kizuri.
Celtic imekuwa mwenyeji wa timu kubwa za bara Ulaya katika kombe hilo katika miaka ya hivi karibuni, lakini hata wale waliokuwepo katika zama za klabu hiyo hawajawahi kushuhudia kipigo kama hicho cha 5-0.
Kasi yao, mafikira na mchezo wao ulikuwa wa kiwango cha hali ya juu.
 
Back
Top Bottom