Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kiumbe huyu ana ulimi mrefu mno ambao humsaidia kula majani ya memea katika miti yenye miba, ni mnyama anayehusudu chakula, anaweza kula hadi kilo 30 na zaidi, pia ni wanyama ambao hawaamini katika kuishi mipakani. Kwa lugha nyepesi ni mnyama anayeishi kwa kuhama hama na hii ni kutokana na kutafuta chakula kwani hutumia chakula kingi, hasumbuliwi na kiu, hivyo maji si jambo muhimu kwake, ikiwa kama atapata majani yenye unyevu nyevu.
 
Ni mnyama mpole anayeamini katika amani, ila hataki kabisa kusikia mambo ya kuonewa na huwa haogopi kitu. Wakati mwingine huamua kukimbia ili kuepusha shari hata kama lililopo mbele yake analimudu, ana ustarabu uliotukuka.

Ngozi yake ni dili kubwa ila chonde chonde usijaribu kwenda kuitafuta kwani anapewa ulinzi mkubwa mno. Ukimuondoa faru na tembo, yeye pia hupewa daraja kubwa la uangalizi.
 
Ngozi yake hutumika kutengenezea nakshi ya mavazi ya wakubwa huko duniani, lakini pia ngozi hiyo hiyo ni tiba kwa wataalamu wetu wa mila huku Afrika.

Ukimuona ni mwembamba lakini ni mzito kupita kiasi, ana kilo zaidi ya 500 na umri wake wa kuishi ni miaka 25, ambapo kama atafikisha umri huo basi tayari atakuwa amefikia viwango vya juu vya uzee.
 
Kwa umri huo, huwa rahisi kukamatwa kizembe na wanyama walao nyama.

Ukiwaona unaweza kuwatofautisha kwa kuwatazama kichwani, dume huwa na pembe fupi ambazo unaweza usizione kama hautakuwa makini kwani huwa na urefu wa nchi tano na jike hukosa kabisa au huchomoza kidogo kutokana na umri.
 
Twiga ni mnyama mrembo mbali na kuwa na haiba ya kuvutia kwa urefu wake, lakini pia ana ngozi yenye rangi nzuri, macho yake ni makubwa na anajua kuyatumia vyema kutazama jambo ambalo humuongezea sifa, katika umri wake wa miaka mitano huwa tayari amepevuka na yupo tayari kwa kumjua dume. Dume huwatambua kwa kunusa mkojo wake, mnyama huyu ana uwezo mzuri wa kukimbia ila ni miongoni mwa wanyama ambao wanajichochea yaani kwa kadiri anavyokimbia ndivyo spidi yake inaongezeka, wenzie wenye sifa hiyo ni mbuni na tembo.
 
Kwa kuanzia na kwa kifupi, tabia ni kanuni zilizo rasmi au zisizo rasmi zinazojengwa kupitia malezi au makuzi. Tunafunzwa tabia njema nyumbani; mfano, namna ya kuheshimu wakubwa, kuishi na majirani, kuwajali wengine, kushirikiana na wengine, namna ya kula chakula kwa adabu, staha katika mavazi na mwenendo, n.k. Shuleni wanafunzi hujifunza nidhamu kama namna ya kuwa na adabu na tabia njema.
 
Back
Top Bottom