wa mfano, wakati wewe unaamini kuwa kuketi juu ya kiti na kula na kijiko ni desturi na tabia njema, ujue kuna wengine wanaona kuketi juu ya mkeka na kula kwa mkono ni desturi na tabia njema. Zote ni sawa kwa sababu tabia hizo zinatokana na utamaduni na kawaida za watu mbalimbali na watu wahusika wanaamini hivyo. Kwa kifupi, tabia njema na zinazokubalika ndio mzingi wa kuwa na mahusiano mazunri na watu wengine. Ukiwa unawakera watu kutoka na tabia au vijitabia vyako, ujue utapata hasara siku moja. Kabla hatujachambua tabia hizo na vijitabia vyenye kukera, ni vizuri tuzijue kanuni muhimu zinazojenga mahusiano mazuri.