Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika mabawa ya ndege huyu kila upande huwa kuna manyoya 16 ya mwanzo,katikati huwa 4 na ya mwisho yanakuwa ni kati ya 20 hadi 23 na kwenye mkia huwa kuna manyoya yasiyopungua 50 hadi 60.



Mbuni anaweza kukimbia kwa mwendokasi ambao hufika hadi takribani km. 70 kwa saa, mwendokasi huu hupelekea mbuni kuwa na sifa ya pekee kabisa kuliko ndege wengine.
 
Mguu wa mbuni una vidole viwili vyenye kucha kwa mbele na kidole cha nje huwa hakina kucha wakati ndege wengine huwa na vidole vitatu hadi vine na uwepo wa vidole hivi humsaidia kuwa na mwendo kasi wa ajabu sana kuliko ndege wengine duniani.
Mbuni akiwa katika mwendo huweza kufikia mita tatu hadi tano, mwendokasi huu huweza kumsaidia mbuni kukimbia panapotokea hatari ya kuvamiwa na adui au kuwahi kwenda kuatamia mayai kama mvua inakaribia kunyesha wakati akiwa mbali.
 
DJru2ahXcAAQmF9.jpg
 
Mabawa yake husaidia wakati wa kukimbia na kuhifadhi joto katika mazingira ya hali ya hewa tofauti kwasababu mbuni hupatikana katika mazingira ya hali ya hewa ya baridi na joto, kwahiyo kunapokuwa na baridi hukunja mabawa ili kuhifadhi joto na kuyapanua kuachia joto litoke wakati wa joto kali.
Mabawa ya ndege huyu hutumika kufunika vifaranga wakati wa mvua, jua kali na hata wakati wa baridi kali na anapopanua mabawa yake huweza kufikia upana wa mita mbili.
 
Back
Top Bottom