Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UMRI WA KUISHI

Duma wanapokuwa maeneo ya hiufadhi huishi kiasi cha myaka 12-14 ila endapo atakuwa anafugwa basi hufikia mpaka umri wa myaka 17.

MAZINGIRA

Duma hupendelea maeneo yalio wazi yenye majani marefu kidogo. Majani haya humsaidia duma kujificha wakati wa kuwinda. Mara nyingi maeneo haya huwa tambarare ambayo pia humsaidia duma kuona mbali zaidi na kuweza kukadiria umbali aliopo mnyama.
 
CHAKULA

Duma ni jamii ya wanyama walao nyama. Miongoni mwa wanyama ambao duma hupendelea sana kuwawinda ni swalatomi, swalapala, watoto wa nyumbu na wanyama wengine wadogo wadogo wenye kwato.
 
SEHEMU WAPATIKANAZO DUMA NA IDADI YAO

Historia inaonyesha kuwa duma walikuwa wanapatikana maeneo yote barani Afrika na sehemu kubwa ya bara la Asia, yaani kuanzia Afrika Kusini mpaka maeneo ya India. Lakini kwa takwimu za sasa duma wanasemekana kusalia maeneo ya Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Kusini magharibi mwa Afrika na sehemu ndogo sana ya Iran.
 
Mpaka kufikia miaka ya 1900, bara la Afrika lilikuwa na duma zaidi ya laki moja. Lakini kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa bara la Afrika wamebaki duma kati ya 9,000-12,000. Huku Iran wakiwa wamesalia duma takibani 200 tu.
 
KUZALIANA

Duma hawana kipindi maalumu cha kuzaliana hivyo huzaa wakati wowote wa majira ya mwaka. Duma jike hubeba mimba kwa muda wa siku 90-100 (mkadirio ya miez 3) na huzaa watoto kati ya 4-6. Watoto wa duma huzaliwa wakiwa na rangi ya kijivu wakiwa na manyoya marefu kama yafananayo na sufu yalio lala upande wa mgongoni. Manyoa hayo huwasaidia pia kujificha kwenye majani kutokana na maadui mfano simba na fisi.
 
Mama huwa na jukumu la kuwahamisha watoto kila baada ya muda siku chache na kutafuta maficho mengine ambayo ni salama. Wiki ya 5-6 watoto huanza kuongozana na mama yao na kula chakula ambacho mama anakuwa amewinda kwa muda huo.
 
Mama hukaa na watoto kwa muda wa miezi 16-18 na baada ya hapo familia hii husambaratika na kisha mama kutafuta dume mwingine kwa ajili ya kuzaa tena.

Watoto wa duma hufikia umri wa kuzaa kuanzia miezi 20-24 (takribani myaka 2). Watoto wengi wa duma huwa wanakufa wakiwa na umri mdogo na hii ni kwasababu mama hulazimika kuwaacha peke yao anapokwenda kutafuta chakula na hapo ndipo fisi, simba, mbwa mwitu au nyati wanapo wakuta huwauwa.
 
UHIFADHI

Duma ni wanyama ambao wamepungua kwa kasi kubwa sana kutokana na changamoto mbali mbali. Hali hii imepelekea wanyama hawa kuingizwa kwenye sheria muhimu za nchi husika katika uhifadhi. Shirika la umoja wa mataifa linalo jihusisha na uhifadhi wa maumbile asili (IUCN-International Union for Conservation of Nature) limewaweka duma katika kundi la wanyama ambao endapo idadi yao itashindwa kuongezeka basi watakuwa ni wanyama waliopo hatarini kutoweka duniani.
 
Ni jambo la kuskitisha sana kuona Afrika Mashariki kwa ujumla tuna duma wapatao 2,572 tu,hii ni hatari sana kwakweli.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKUMBA DUMA

Migogoro kati ya binadamu na wanyama hasa jamii za wafugaji kwa duma wanao ishi nje ya maeneo ya hifadhi wamekua wakiuliwa sana pale wanapo shambulia mifugo ya watu.
Shughuli za uwindaji ambazo hupunguza idadi ya wanyama tegemezi kwa duma hivyo kufanya wanyama hawa kuwa na njaa kwa muda mrefu.
 
Duma wana naswa sana na wanya ambazo hutegwa na majangili kwa ajili ya kukamata wanyamapori hivyo kufia mitegoni bila msaada.
Ajali za barabarani hasa kwa barabara zilizo pita ndani ya hifadhi mfano Hifadhi ya Taifa Mikumi na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na hata zile zilizopo karibu na maeneo ya hifadhi. Magari yamekua ya kigonga sana wanyama hawa kutokana na mwendokasi wa mabasi usababishwao na maderva wazembe.
 
Idadi kubwa ya magari ya watalii hifadhini. Duma ni wanyama ambao wanavutia sana kuwaangalia hivyo anapoonekana sehemu watalii huitana na kujaa sehemu moja hivyo kuwafanya duma kukimbia kwa hofu.
Uchimbaji rasilimali asili mfano madini na mafuta vimepelekea sana kuharibu mazingira na hivyo kuwafanya duma kutoweka baadhi ya maeneo.
 
Ujangili ulio kithiri ambapo duma huwindwa kwa ajili ya ngozi na sehemu nyingine za mwili kama kucha na meno. Hii yote husababishwa na biashara haramu ya wanyamapori na malighafi zao.
SIASA- huu ni ugonjwa mkubwa sana katika uhifadhi wanyamapori na mfano mzuri ni hapa nchini kwetu. Mbunge anadiriki kusema kuwa Tanzania tuna maeneo mengi yalio tengwa kwa ajili ya uhifadhi na kudai kwamba kwanini wananchi wasipewe maeneo hayo wakalima. Aibu kubwa hii kwa msomi pia mbunge tegemezi kwa jamii za watanzania.
 
NINI KIFANYIKE KUWANUSURU DUMA HASA HAPA TANZANIA

Viongozi waepuke kuleta siasa kwenye uhifadhi kwani wakumbuke kua wao ni wakupita tu ipo siku wataondoka ila wanyamapori watabaki tu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Kutafuta njia sahihi ya uvunaji rasilimali asili bila kuharibu mazingira ya wanyama maeneo ya hifadhi.
Kuwep kwa elimu ya uhifadhi mashuleni, uzalendo na kuongeza idadi ya askari wanyamapori ili kutokomeza tatizo la ujangili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…