Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

080ec91ba7340dab649f77d2f96bdb60.jpg
 
1.Ni mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula chakula chochote. Wana uwezo wa kuishi katika mazingira magumu. Aina moja kwa jina Eublaberus posticus wanaweza kuishi mwaka mmoja kwa kunywa maji pekee
2.Ni mdudu anayeweza kuishi wiki mbili bila ya kunywa maji.
3.Wakati moyo wa mwanadamu ni mmoja wenye chemba nne mende ana moyo mmoja wenye chemba kumi na tatu.
 
4.Baadhi ya mende wa kike hawaitaji wanaume kuweza kuzalisha mayai hupandana wao kwa wao na kutaga mayai katika kipindi chote cha maisha yao.
5.Mende ana uwezo wa kukaa kwa zaidi ya dakika 40 bila ya kupumua.
6.Mende ana uwezo wa kuishi zaidi ya wiki mbili akiwa amekatwa kichwa.
7.Ana uwezo wa zaidi ya mara 15 ya binadamu wa kuzuia miale mikali ya nuklia isimdhuru na kubaki hai. 8.Mende ni mdudu asiye na mapafu.
 
9.Ana uwezo wa kuruka maili 3 kwa saa.
10. Badala ya kuwachukia, wanasayansi huwafurahia sana na kuwatumia kwa manufaa ya binadamu. Mwaka 1999, mende walitumiwa na Prof Robert Full katika Chuo Kikuu cha California, Berkley, kumpa wazo la kuunda roboti ya miguu sita iliyosonga upesi na kwa urahisi.
 
11. Mende wanatumiwa pia katika matibabu. Wanasayansi kwa miaka mingi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wa mende kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika. Wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupigana na sumu. Leo katika hospitali Uchina, krimu inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosiagwa hutumiwa kutibu vidonda vya moto na pia humezwa kutibu vidonda vya tumbo
 
Ukiitazama sura ya dunia hasa nchi kavu utakutana na milima na mabonde, ipo milima ya aina mbalimbali kutokana na namna ilivyofanyika mpaka kufikia hapo ilipo!! Milima ni miinuko ambayo ina urefu kuanzia mita 600 toka usawa wa bahari!
 
Mlima Kilimanjaro ni wa 10 kwa urefu duniani ukiwa na futi 19,317.
Milima imekuwa chanzo cha kufanyika mvua kwa kulazimisha upepo wenye mvuke kupanda juu na baadaye kusababisha mvua nyingi katika upande unaopakana na bahari (Windward side), huku upande wa pili ( Leeward side ukipata mvua chache au kukosa kabisa.
 
Pamoja na kutokea kwa mmomonyoko wa udongo (soil erosion) unaosababisha na mvua na upepo milima imekuwa ikipungua kwa kiasi kidogo sana, kuna wanasayansi wanaoamini katika kinachoitwa "Isostacy theory"
 
NIKUPE VIONJO KADHAA KUHUSU MASHOTO
1. Mashoto wana uwezo mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu kiasi kwamba wengi wao hawatumii shajara (diary) na hawapendi kutumia notebooks wanapomsikiliza mtu akitoa mhadhara. Utagundua kuwa katika maisha yako ya shule wengi wa MASHOTO ambao ni vipanga si wasomaji wa kukomaa sana/kukesha nk.
 
Back
Top Bottom