Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sakata la @hamisamobetto... @zarithebosslady Lazidi kuwagusa Watu kibao... Time hi shilole yamemfika hapa.. Ameamua kutoa povuuu : . By @shilolekiuno_badgirlshishi Mwanamke asiyejielewa ndio huwa hutumia mwili wake kujidharirisha na kuwatumia watoto malaika wasio na kosa kutafutia kiki. Mwanaume akikupenda atakuweka ndan atakuthamini. Kinyume na hapo mtatumiana kwa maslai yenu binafsi. Ukiwa mwizi unakuwa hata na heshima kwa mwenye mali yake yann mpk udhalilishwe na mwanaume ijulikane hupendwi ila umetumiwa tu. Vinginevyo hata huduma unayopata kwa wiki utaisikia bombani. Kwani haiwezekan mwananke kufighty na kutulia na watoto wako mpk utengeneze drama? Hebu tubadiliken jmn huu u GOLD DIGGER unatudhalilisha tu. Aaagh mi nakereka tu hebu niendelee na umama ntilie wangu au sijui na mm niwatafute wababa wa watoto zangu tuanze drama Post hii haisuani na lolote wala chochote sitaki povu hapa leo nimeamka na vya Igunga kichwani. - 8
 
MFAHAMU MBWA MWITU
Mbwa mwitu ni wanyama wawindaji wanaokula nyama, ni wanyama wafupi na wadogo kimuonekano, huishi katika makundi makumbwa sana, urefu wa kutoka miguuni hadi begani huweza kufikia inches 35 tuu na hiyo ni kwa wale ambao wakubwa, lakini urefu wa kichwani mpaka mkiani hufikia inches 55, kwa vipimo hivi unaweza kuona wanyama hawa ni wadogo kiasi gani kwa maumbo yao, lakini kama vipimo hivyo ni mtihani basi kukurahisishia nakwambia hivi, mbwa mwitu kwa umbo ni mdogo zaidi kwa mbwa tunaowafuga.
 
Wanyama hawa huishi katika vichaka na sehemu majani makavu makavu, hubeba mimba kwa miezi mitatu na siku chache kidogo kama atazidisha, na hawana idadi maalumu ya watoto anaozaa hapa hutegemea dume lilikuwa na mbavu kiasi gani, lakini kwa kifupi huzaa watoto wengi, watoto hukaa chini ya uangalizi wa mama kwa kwa miezi mitatu na baada ya hapo huanza kujitegemea, wanapofikisha mwaka mmoja majike huanza kunusa harufu ya kuitwa mama, maana huanza kuyadondosha mate madume, kwa muonekano wao mzuri na wakuvutia.
 
Viumbe hawa huishi kwa miaka kumi tuu na wakizidisha wanaweza fikisha miaka 12, huishi kwa kuendeleza koo zao, na wanafahamiana vyema kwani wanyama hawa ni wapenzi Sana wa kushirikiana, na walinzi wazuri wa mipaka yao.
 
Tabia yao ya umoja, kushirikiana huwafanya waonekane ni wababe wa mji, wanyama hawa huogopwa hata na wanyama wenzao wanao winda kwani bifu lao huwa ni lakufunga mtaa, hata simba akiwaona mkia wake huuficha, usiseme kwa fisi nk, huweza kukimbia umbali wa km 71 kwa saa, hivyo kaa ukijua ni viumbe ambao wana hatari sana wakati mwingine humla mnyama wakati wanamkimbiza.
 
Mbwa mwitu wapo wa aina mbili ninaowafahamu wapo hawa ninaowazungumzia ambao kwa lugha ya mama Theresa wanaitwa wild dog, na wapo aina nyingine wanaitwa wolf, tulio nao hapa nyumbani ni hawa wild dog, wolf hatuna katika mbuga zetu.
 
Tofauti yao huanzia katika muonekano, mbwa mwitu wa kwetu ni wadogo sana katika maumbo, wakati wolf ni mbwa mwitu wakubwa sana pengine kuliko tunaowafuga, mbali na muonekano lakini pia majuku yao hufanya kwa staili tofauti, wakati mbwa wa kiAfrika wanapokwenda kuwinda wakiongozana pamoja na kufukuza pamoja windo lao, wolf hugawana njia na mmoja wao anapoona windo huanza kwa kulizubaisha akilikenulia meno na kutoa sauti ambayo wenzao hutambua kuwa wanaitiwa nini,
 
wolf ni mnyama anayevutia na anamuonekano mzuri sana na rangi zao ni nzuri sana ukimuona unaweza tamani umkumbatie lakini roho yake ni ya kinyama sana hana huruma hata chembe ni heri ukutane na simba, mbwa mwitu wetu wana sura mbaya hawana rangi nzuri lakini kwa binadamu wana utu sana hawezi kukuvamia pasina sababu, wakati wolf ni viumbe ambao kwa mbio wanaweza fata kwa duma, ndio kwanza mbwa mwitu wetu hawana mbio sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…