Ni muhimu kuwa na vifaa vya huduma ya kwanza nyumbani kwa ajili ya kumhudumia mtu aliyeumia / kuugua ghafla kabla ya kumpeleka hospitali. Pia ni vyema kila mzazi na mlezi akawa anajua angalau kidogo kuhusu huduma ya kwanza hasa kwa watoto.
Dawa ya kuoshea mahali palipoumia (Dettol ya maji, Eusol)
Dawa za kupunguza maumivu ( Panadol, Dicloper etc)
Mafuta ya kupaka sehemu ndogo iliyoungua
Dawa ya kukatisha kuharisha
Thermometer
Namba za simu za dharura ( daktari, fire, polisi, mchungaji, ofisini n.k )
Majanga ya moto ni majanga y a hatari sana katika nyumba zetu. Majanga mengine yapo nje ya uwezo wetu ila kuna mengine tunayoweza kuyaepuka kwa kuwa waangalifu na makini zaidi. Majanga mengi ya moto majumbani hutokana na majiko ya mafuta ya taa, mishumaa, vibatari, matatizo ya umeme na majiko ya kuni.
Uwepo jikoni hadi umemaliza kupika chakula chako, unapoacha jiko linawaka na wewe upo mbali ni rahisi sana kutokea madhara.
Weka vitu mbali na jiko ili kuepuka kushika moto na kuunguza nyumba.
Hakikisha watoto wadogo hawaingii jikoni wakati unapika ili kuepuka ajali hasa wanaotambaa.
Unapopikia jiko la kuni au mkaa hakikisha umezima kabisa moto wote kabla ya kuondoka jikoni.
Zima mtungi wa gesi unapomaliza kupika hasa kama una watoto wadogo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.