Siafu ni wadudu ambao kila mmoja wetu ameshawahi kukutana nao au anawafahamu. Siafu ni wadudu wa ajabu sana wenye umoja,ushirikiano na jitihada sana. Jamii ya Siafu imegawanyika makundi 3 ; Malkia , wanawake na wanaume. Mtafiti mmoja wa chuo kikuu cha Arizona anasema " katika jamii ya Siafu wafanyakazi na malkia
Siafu ni wadudu ambao kila mmoja wetu ameshawahi kukutana nao au anawafahamu. Siafu ni wadudu wa ajabu sana wenye umoja,ushirikiano na jitihada sana. Jamii ya Siafu imegawanyika makundi 3 ; Malkia , wanawake na wanaume. Mtafiti mmoja wa chuo kikuu cha Arizona anasema " katika jamii ya Siafu wafanyakazi na malkia ni wanawake"
Kuna jamii za Siafu duniani zaidi ya 120000, ajabu ni kwamba Siafu anaweza kubeba mzigo mzito mara 20 zaidi ya uzito wake mwenyewe.
Pamoja kwamba Siafu ni wadogo lakini wanampangilio na umoja wa ajabu, inaaminika Siafu wamesambaa duniani pote isipokuwa bara la Antactica.
Malkia wa Siafu anapokufa basi jamii hiyo haitachukua muda mrefu nayo itakufa⚰ au kupotea.
Jamii ya siafu yenye utawala wa malkia mwenye nguvu hupanuka na kufikia hatua ya kupigana⚔ na jamii nyingine za Siafu na kuwateka mateka na kuwatumikisha.
Jamii inayotekwa haishii kufanywa watumwa tu ila hata mayai yao hutunzwa kuanguliwa na watoto wao huendelea kuwa watumwa daima.
Kitu cha kushangaza sana Siafu hufanya kazi kwa shift na pia kupumzika wanasayansi hawajapruvu kama wanakuwa wamelala ila imegundulika hupumzika kwa kupunguza shughuli zao.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.