Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jambo la msingi katika uhusiano wa tiba ni kujenga mazingira ya kuaminiana na kutunza siri kuhusu habari njema zinazopatikana katika mazingira ya tiba. Kabla ya kutafuta daktari wa kukutibu, lazima ujiulize swali hili: “Je! ninamwamini daktari huyu?”
 
Ukweli ni kwamba, uzoefu wa kazi, mara nyingi madaktari hubaini uongo wa wagonjwa na wakati mwingine jambo hilo huwakatisha tamaa na kuwavunja moyo wa kutoa msaada stahiki.

Madaktari wengi wanapobaini uongo wa wagonjwa, hujisikia vibaya kwani huona kuwa, wao si muhimu kwa mgonjwa husika.
 
Uongo wa mgonjwa usipobainika, unaweza kumfanya daktari kutoa matibabu yasiyo na msaada au yanayohatarisha afya ya mgonjwa. Madaktari hushindwa kutambua matatizo ya wagonjwa na kutoa tiba sahihi na salama, pale wanapopewa taarifa zisizo sahihi.
 
Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa, idadi ya wagonjwa wanaowadanganya madaktari kuhusu afya zao au kuzuia baadhi ya taarifa muhimu ni kubwa kufikia kiasi cha mgonjwa mmoja kati ya wanne. Hii ni sawa na asilimia 25 ya wagonjwa wanaoenda hospitalini kila siku.
 
Hii hujitokeza zaidi kwa magonjwa yanayosababisha unyanyapaa, mapenzi ya jinsi moja, idadi kubwa ya wapenzi, utoaji wa mimba, uvutaji wa sigara, matumizi ya pombe, dawa za kulevya, matumizi ya ugoro pamoja na kuchanganya dawa za asili na zile za hospitalini.
 
Mara nyingi hali hii hutokea kama mgonjwa atahisi kuwa daktari au mhudumu wa afya atamhukumu kimaadili. Pia wagonjwa wengine hupenda kuwafurahisha madaktari ili wasichukie kwa kufikiri kuwa wagonjwa hawafuati kwa makusudi maelekezo sahihi ya tiba wanayopewa.
 
Wagonjwa pia, hujikuta wakiwaambia madaktari uongo kwa kupunguza uzito, kujifanyisha au kuongeza chumvi kwenye matatizo yao ya kiafya.

Lengo huwa ni kuvuta usikivu wa madaktari kwa matazamio ya kupata huduma bora zaidi. Wagonjwa wengine pia huwa na matazamio ya kuandikiwa vipimo au dawa fulani na anapomshauriwa au kupewa vipimo na dawa tafauti, mgonjwa anaweza kumwambia daktari kuwa dawa hiyo inamsababishia matatizo wakati si kweli.
 
Jambo ambalo kila mwanamke anapaswa kulifahamu ni kwamba, yapo mambo ambayo anaweza kuona kama tatizo la kawaida au lisilohusiana na ugonjwa wake na akalifanya kuwa siri, lakini kumbe ni dalili muhimu ambayo ingemsaidia daktari kugundua tatizo kubwa la kiafya linalomsumbua au lililoko njiani kumuathiri.
 
Yapo mambo mengi, lakini hapa nayataja kumi. Hayo ni mwanamke anapohisi maumivu wakati wa kujamiiana, kuota nywele nyingi mwilini au ndevu, kukosa hamu ya tendo la ndoa, maji yenye harufu mbaya kutoka ukeni, kuwa mjamzito, hamu ya tendo la ndoa kupita kiasi, uvimbe njia ya haja kubwa, kuota kinyama kwenye njia ya haja kubwa, tabia ya kufanya mapenzi kinyume cha maumbile na kutumia vipodozi haramu.
 
Mengine ni mwanamke kuficha kuwa anatumia njia za kupanga uzazi au ana ujauzito, jambo ambalo linaweza kumfanya daktari kumwandikia dawa ambayo inaweza kumuathiri au kulingana na hali halisi iliyopo.

Mwanamke anaweza akawa ameathirika kwa vipodozi lakini humficha daktari akiamini atampatia dawa ambayo itamtibu. Hali hii inaweza kumfanya asipone haraka kwa kutopata dawa mwafaka au akaathirika zaidi kutokana na kuendelea kuvitumia vipodozi vyenye sumu
 
Wapo wanawake ambao pia hushindwa kuwaeleza madaktari ukweli kuhusu mzunguko wao wa hedhi na kiasi cha damu wanachopata kila wanapoingia kwenye mazingira hayo kila mwezi. Hii ni njia mojawapo inayoweza kuonyesha ishara au dalili fulani ambayo ni muhimu kwa daktari kurahisisha uchunguzi wa matatizo yanayomkabili mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…