Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Anapohisi maumivu wakati wa kujamiiana, inaweza kuwa dalili ya matatizo makubwa kama vile Uambukizo katika Mfuko wa Uzazi (PID), uvimbe tumboni (Fibroid), kugandamana kwa via vya uzazi (pelvic adhesions) au kuota kwa misuli ya mfuko wa kizazi sehemu zingine za mwili (Endometriosis). Mambo hayo yanaweza kusababisha mimba kutunga nje ya kizazi au mwanamke asipate ujauzito.
 
Mwanamke kuwa na nywele nyingi mwilini, kuota ndevu nyingi au kuwa na ukavu wakati wa tendo la ndoa inaweza kuwa ni dalili ya tatizo la kukosekana kwa ulinganifu wa vichocheo vya jinsi mwilini.

Kinachoweza kuchochea pia matatizo haya ni uvimbe katika tezi za mayai. Mara nyingi matatizo ya tezi za mayai ya mwanamke husababisha ugumba.
 
Zamani tulizoea kuona wanawake wakifanya kazi nyepesi nyepesi huku baadhi zikionekana za wanaume kutokana na uhitaji wake wa nguvu nyingi katika kuzifanikisha.

Lakini, hali ni tofauti na hivi sasa kwani tumeona wanawake wameweza kujichanganya na kuacha kuchagua kazi na bila kujali mazingira wala jamii inavyowachukulia.
 
Hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya wanawake wakijitosa katika kuendesha mabasi ya kusafirisha abiria au malori ya kupeleka mafuta nje ya nchi.

Wanawake wengine wamejitosa katika kazi ya utingo wa daladala na wengine kuwa makondakta kwenye magari hayo yanayotoa huduma ya usafiri ndani ya jiji.
 
Utingo wa daladala jijini Dar es Salaam, Margaret Joseph (30) anasema katika kuangalia wapi atapata ridhiki aliamua kujaribu kazi hiyo.

Mama huyo wa watoto wawili anasema licha ya watu kumsema kuwa kazi hii haiwafai wanawake, hakujali kwa kuwa anaamini mwanamke anaweza kufanya chochote.
 
Awali nilikuwa nafanyabiashara ya mama ntilie, lakini baada ya kuona sipati faida niliamua kutafuta kibarua ndipo nilipoona nijaribu kufanya kazi hii,” anasema Mage kama anavyoliita jina lake kwa kifupi.

Akisimulia mkasa huo anasema siku ya kwanza alipokwenda kuomba kazi alikutana na utingo mwenzake katika gari hiyo na kumueleza nia yake jambo lililomshangaza. “Utaweza? aliniuliza mara kadhaa huku akioneka mwenye mashaka, lakini baadaye alikubali na mimi kuanza kazi,” anasema Mage.
 
Haikuwa rahisi kuzoea mazingira ya kazi hiyo haraka kwani alikuwa akiona aibu kuita watu pindi anapofika kituoni jambo lililofanya baadhi waliogundua hali hiyo kumtia moyo.

Anasema kupitia kazi hiyo kwa sasa amekuwa na kipato kinachotosha kukidhi mahitaji bila shida yoyote.
 
Naye Jenipher Msaki (29) mama wa watoto wawili anasema aliingia katika kazi hiyo baada ya ‘kuharibiwa maisha’ na mwanaume aliyekuwa akiishi naye.

“Nilikuwa nimejiajiri katika kibanda changu cha M-Pesa kilichokuwa kinanisaidia na familia yangu katika kupata mahitaji ya nyumbani, lakini baada ya kuolewa nilijikuta nikipoteza kila kitu na kuona ni bora kuishi mwenyewe kuliko kupotezewa muda zaidi,” anasema Jenipher.
 
Anasema baada ya kukaa miezi kadhaa bila kufanya kazi na kukosa chochote cha kuhudumia familia, aliamua kutafuta kazi ya kufanya alijikuta ametumbukia katika kazi hiyo.

Anasema baada ya kuanza kufanya kazi hiyo ndani ya miezi mitatu aliweza kujikimu kwa kupanga chumba, kuhudumia familia na kuwapa watoto mahitaji yote muhimu.
 
Back
Top Bottom