Awali nilikuwa nafanyabiashara ya mama ntilie, lakini baada ya kuona sipati faida niliamua kutafuta kibarua ndipo nilipoona nijaribu kufanya kazi hii,” anasema Mage kama anavyoliita jina lake kwa kifupi.
Akisimulia mkasa huo anasema siku ya kwanza alipokwenda kuomba kazi alikutana na utingo mwenzake katika gari hiyo na kumueleza nia yake jambo lililomshangaza. “Utaweza? aliniuliza mara kadhaa huku akioneka mwenye mashaka, lakini baadaye alikubali na mimi kuanza kazi,” anasema Mage.