Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alizaliwa mwaka 1973 katika kijiji cha Madaba mkoani Iringa,ambapo alipata kuspoma katika shule ya msingi Mdaba,nakumaliza darasa la saba hapo,hakubahatika kujiunga na elimu ya sekondari kutokana na kipato kidogo kutoka katika familia yake
 
Alianza kazi za umama ntilie Maeneo ya posta mwaka 2009,ambapo hakuweza kudumu kufanya kazi ya kuuza chakula maeneo hayo kutokana na vurugu za askari wa jiji kuwatimua na hivyo kujikuta akiwa katika wakati mgumu wa kupata eneo maalumu ya kufanyia kazi yake ya mama ntilie,akiwa na mtoto wake ambaye alikuwa anasoma shule ya msingi
 
Baada ya kuhaha kwa muda mrefun alipata maeneo tandale,Manzese na mabibo,hatimaye kupata eneo japo halitoshelezi lakini ndiyo mahali anapaendesha majukumu yake yakijasiliamali.Kwa mika 6 amekua akipika chakula na kuuza kazi ambayo yeye anaizungumzia ni kazi
 
Akizungumzia changamoto anazokumbana nazo,mama Sodana anasema kwakua kazi kubwa ya kupika amekua akiifanya kwa kuwapikia wananfunzi wa chuo,amekuwa akikutana na changamoto kwa baadhi ya wateja kula pasipo kulipa na wengine kuondoka na ela yake jambo ambalo limekuwa likimrudisha nyuma kimaendeleo.
 
Mama Sodana anafunguka kwa kusema kuwa faida na mafanikio ambayo anayapata siyo makubwa sana lakini anaridhika kwa kidogo anachokipata,na kinamuwezesha kumsomesha mwanae ambaye anasoma sekondari,mabli nahilo ameweza kujinunulia shamba kijijini kwao,pia kuweza kulipa pango la nyumba na mahitaji mengine ya kibinadamu.
 
Kuhusu mauzo ya chakula,mama Sodana ansema kuwa kwasiku anaweza kuuza sahani 20 za ugali na 20-25 kwa sahani za wali kutokana na biashara yake inategemea sana wanafunzi wa chuo,jambo ambalo halitoi ongezeko la pato kutokana na idadi ya wananfunzi kupungua na kuongezeka kwa misimu,ambapo
 
Lkini pia nilimuuliza kuhusu kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii,alisema kuwa ,kwa yeye hajui chochote kuhusu hilo,na wala hajui taasisi hizo zinavyofanya kazi,kwahiyo ameyoa wito wa elimu ili aweze kujiunga na na kunufaika na mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…