Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa mengineyo kama kisukari.
 
Watafiti hao wameeleza kuwa, kuwa na mafuta kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo makubwa ya umetaboli.
Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba, ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno
 
Ingawa suala hilo linaonekama kana kama ni kinyume, lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko kuna faida kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi hutoa mada inayoitwa cytokines ambayo huleta uvimbe katika mwili. Mada za cytokines zinahusiana moja kwa moja na magonjwa ya moyo na kisukari. Kuyeyuka taratibu kwa mafuta katika mapaja pia husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na jinsi mafuta yanavyochomeka
 
Kuwa na mafuta mengi katika mzunguko wa tumbo na kuwa na umbo mviringo kama 'tufaha' kunaongeza hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo na sukari. Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko unene wa tumbo.
 
Ameongeza kuwa, katika ulimwengu wa kawaida pia watu huonekana vyema wanapokuwa wanene mapajani, iwapo tu tumbo linakuwa dogo. Daktari huyo ameeleza kuwa, uchunguzi huo umewasaidia kufahamu vyema mafuta katika mwili ili kutafuta mikakati mipya ya kupunguza magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…