Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwiki ni kitendo kisichozuilika ambacho hutokana na kusinyaa kwa kuta za kiwambo cha moyo au diaphragm. Kwa kawaida kwikwi ni kitendo kinachojirudia rudia mara nyingi. Sauti ya 'hic' inayotokea wakati unapokuwa na kwikwi husababishwa na kidaka tonge (epiglottis) ambacho hufunga haraka wakati hewa inapoingia kwenye koo. Kupiga kwikwi kwa kawaida hakuna maumivu lakini mara nyingine husumbua hasa inapoendelea kwa muda mrefu.
 
Kwikwi ya kawaida huweza kutulizwa kwa kunywa maji, lakini wakati mwingine kufanya hivyo hakusaidii.
Zifutazo ni sababu zinazoweza kukuletea kwikwi
1. Kula kwa haraka.
2. Kula chakula cha moto na kunywa maji baridi baada yake.
3. Kulia au kukasirika.
4. Kula chakula chenye viungo vingi au pilipili.
 
5. Kula chakula cha moto sana.
6. Kunywa pombe au soda kwa wingi.
7. Kukohoa sana.
8. Kucheka kupita kiasi.
9. Kufurahi sana, kusisimka au kupatwa na msituko.
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, vitu ambavyo vinakiletea karaha kiwambo cha moyo au diaphragm husababisha kwikwi. Kuna sababu nyingi ambazo husababisha jambo hilo na hizo tulizotaja hapo juu ni miongoni mwazo,ambapo matokeo yake ni humfanya mtu apige kwikwi.
 
Kwikwi kwa kawaida huisha baada ya dakika chache au hata sekunde. Lakini iwapo kwikwi itaendelea kwa masaa au kwa siku, huweza kuwa ni tatizo muhimu la kitiba na pengine hali kama hiyo inaweza ikawa inasababiswa na ugonjwa.
Kuna baadhi ya watu hupata kwikwi sana wakati wa ujauzito, baada ya kufanyiwa operesheni na hata watoto wachanga pia hupatwa na kwikwi mara kwa mara.
 
Wajawazito hupata kwikwi sana mwishoni mwa miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito na mwanzoni mwa miezi mitatu ya pili. Kwikwi hutokea wakati wa ujauzito ni kwa sababu wakati huo uwezo wa kuvuta hewa ndani ya mapafu na kutoa nje huongezeka kwa asilimia 30 hadi 40 ikilinganishwa na hali ya kawaida.
 
Homa hutokea pale joto la mwili linapopanda. Kitaalamu joto la mwili hupanda pale linapozidi nyuzi joto 37 au Farenheit 98.6 kwa kipimo kinachokuliwa mdomoni au nyuzi joto 37.2 au Farenheit 99 kwa kipimo kinachochukuliwa katika makalio (rectal temperature). Hata hivyo kipimo cha wastani na joto la mwili huweza kupanda au kupungua kwa nyuzi joto 0.6 au Farenheit 1 kutoka Farenheit 98.5.
 
Joto la miwli huweza kuongezeka kwa nyuzi joto 0.6 au Farenheit 1 wakati wa mchana. Kwa hivyo homa haichukuliwi kuwa ni hatari hadi pale joto la mwili llinapozidi nyuzi joto 38 au Farenheit 100.4. Homa inasaidia mwili kujilinda na bakteria na virusi ambavyo haviwezi kuishi katika joto kali. Kwa sababu hiyo, joto la chini kwa kawaida halitibiwi, hadi pale linapoambatana na dalili mbalimbali nyinginezo.
 
Homa ni dalili mojawapo ya ugonjwa, na mara nyingi haizingatiwi hadi pale inapoandamana na dalili nyinginezo kama kukohoa, kuvimba koo, maumivu na kadhalika. Homa ya kufikia nyuzi joto 40 au Farenheit 104 inahitajia matibabu ya haraka, kwani isipotibiwa huweza kusababisha matatizo ya ubongo yanayopelekea kutapatapa usingizini kama vile kuota njozi au mawenge,
 
pamoja na degedege hasa kwa watoto.
Themometa za dijitali zinaweza kutumika kupima joto kwa njia ya mdomoni, kwapani au katika makalio. Wataalamu wanashari ni bora isitumiwe themometa ya glasi yenye mekyuri, na ni bora wazazi wasiwe na themometa za aina hizo majumbani ili kuzuia hatari ya mada hiyo hatari yenye sumu.
 
Ni muhimu kutambua kuwa kipimo cha joto kinachochukuliwa kwapani si sahihi sana kikilinganishwa na kile cha mdomoni na makalioni (rectal) na kwa kawaida huwa pungufu kwa nyuzi joto moja kuliko kile kinachochukuliwa mdomoni.
 
Haya tena ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni!...uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani, katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya.
 
Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe. Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makaliao makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo hayasaidii chochote.
 
Back
Top Bottom