Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-09-27-23-45-35.png
 
Matumizi sahihi ya dawa ni nguzo muhimu sana katika kuhakikisha unapona kabisa ugonjwa wako tena kwa njia nzuri na amani. Endapo utaacha kutumia dawa hata kama utahisi umepona au umepata afadhali kinachoweza kutokea ni ugonjwa kutopona kikamilifu au kutopona kabisa na kuweza kujirudia baada ya muda. Pia vijidudu vya magonjwa vinajijengea usugu na kuweza kukwepa dawa na kushindwa kuuliwa na dawa. Hatimaye ni kujirudia kwa ugonjwa, kushindwa kupona vizuri na magonjwa kuwa sugu.
 
Dawa zote kabla ya kuamuliwa zitumikaje zimefanyiwa tafiti na majaribio ya kutosha ndipo ukafikiwa muafaka kuhusu dozi iwe vidonge vingapi, itumike kutwa mara ngapi na kwa siku ngapi au kwa muda gani. Tafiti na majaribio hayo yalifanywa na wanasayansi wenye uelewa, elimu na ujuzi mkubwa sana kiasi kwamba maelekezo hayo ndio njia sahihi kuliko zote ya kutumia dawa hizo na kupata matokeo mazuri.
 
Tumia dawa kama ulivyoelekezwa. Usitumie dawa kwa kujisikia au kwa kuangalia gharama. Kama huwezi kutumia dawa kama inavyotakiwa basi ni bora usitumie kabisa dawa hiyo. Usianze kutumia hata kidonge kimoja!
 
Utafiti umeonyesha kwamba faida ya kucheka ni kubwa na inayofaa kwa afya ya mwili na akili. Watafiti hadi sasa wamedokeza kuwa kicheko husaidia kupunguza maumivu, kuleta furaha zaidi, na hata kuongeza kinga. Kicheko kwa hiyo, ni dawa isiyo na gharama ambayo kila mmoja anaweza kuipata. Kinachotakiwa ni kujenga mazoea ya kufurahi na kujitahidi kuwa na hisia ya ucheshi mara kwa mara. Faida za kicheko:
 
1.Homoni: Kicheko hupunguza kiwango cha homoni zinazoleta msongo(stress) kama cortisol na epinephrine dopamine (Adrenaline). Pia huongeza kiwango cha homoni ya kuimarisha afya kama endorphins na neurotransmitters. Kicheko husababisha kuongezeka kwa idadi ya seli za kinga (antibody); pia huzalisha na huongeza ufanisi wa seli T
 
Yote hii ina maana kuwa mfumo wa kinga mwilini huimarika, na hupunguza uwezekano wa msongo wa mawazo(Stress). 2.Mwili kujiachia(Physical release): Baada ya kicheko akili na mwili hupata hisia nzuri, ni kama unajiachia 3.Utendaji wa ndani Kicheko hutoa mazoezi ya kiwambo (diaphragm), husaidia mabega (works out the shoulders) na kufanya misuli kushirikiana zaidi;lakini pia husaidia moyo(provides a good workout for the heart). Kicheko pia huondoa hasira, hatia, dhiki na hisia hasi.
 
4.Kijamii Kicheko hutuunganisha na wengine. Kucheka hujenga mahusiano mema na huleta kuaminiana.Furaha na faida ya kicheko huongezeka maradufu ikiwa watu wengi wanacheka pamoja.Kicheko ni njia nzuri ya kufahamiana na kushirikiana. Unaweza je kucheka: Kicheko ni moja ya tiba mbadala ya bure, urahisi na yenye manufaa kwa njia nyingi. Unaweza kupata zaidi kicheko katika maisha yako kwa mikakati ya ifuatayo:
 
1.Angalia vipindi vya TV vya kuchekesha pamoja na filamu za ucheshi. 2.Cheka na marafiki kazini,shuleni na hata nyumbani. Fanya kicheko kuwa tabia yako. 3.Acha kulalamika kuhusu maisha,jaribu kucheka. Kama jambo fulani linakuchanganya ni vizuri kuangalia nyuma juu yake na kucheka. Usikubali kusongwa na mawazo,zungumza na wenzako lakini juu ya yote angalia,soma au kumbuka mambo yatakayokuchekesha ! Wachaaaa nichekeeee mieeeee Haaahaaaa ahaaaaaaa....Yeeaaaaaahhh
 
Kuna mjadala wa muda mrefu kuhusu suala la nyama nyekundu, ambapo makundi mawili tofauti yamekuwa yakitoleana hoja kuhusu faida na madhara ya kula nyama, hasa ile nyama iliyowekwa katika kundi la ‘nyama nyekundu’ (red meat).
 
Wakati wakereketwa wa masuala ya afya wanasema kuwa nyama nyekundu huchangia hatari ya mtu kupata ugonjwa wa moyo na saratani ya tumbo, wadau wa nyama wanadai kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya saratani, ugonjwa wa moyo na nyama nyekundu.
 
Wakereketwa wa masuala ya afya wanaeleza kuwa ukweli uko wazi kwamba nyama nyekundu inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo kwa mtumiaji, kwani baadhi ya nyama nyekundu huwa na kiwango kikubwa mafuta (saturated fat) ambayo huongeza kolestro mwilini na mtu mwenye kiwango kikubwa cha kolestro huwa hatarini kupatwa na ugonjwa wa moyo.
 
Kwa upande wa saratani, watafiti wanasema kuwa bado hakujawa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa nyama nyekundu inaweza kusababisha saratani ya tumbo. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Afya ya Taifa nchini Marekani, umebaini kuwa watu wanaopenda kula kwa wingi nyama nyekundu, hufa mapema kuliko wale wanaokula kiasi kidogo cha nyama hiyo.
 
Back
Top Bottom